loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa: Mv Victoria ianze kazi

Majaliwa: Mv Victoria ianze kazi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza meli ya MV New Victoria Hapa Kazi tu ianze kazi wiki ijayo kusafi risha abiria na mizigo kwa kuwa ukarabati umekamilika na inaendelea kukaa tu hivyo kuisababishia hasara Serikali.

Majaliwa ametoa siku mbili kwa mamlaka inayohusika kutoa kibali cha kuanza kazi kwa meli hiyo kuhakikisha inakitoa haraka na pia ratiba ya safari itangazwe kwa sababu Watanzania wana hamu ya kuanza kuhudumiwa na meli hiyo.

Alitoa maagizo hayo jana baada ya kukagua ukarabati mkubwa ulifanyika katika meli hiyo ambayo tayari imefanya safari ya majaribio kwa ufanisi mkubwa kwa kusafirisha abiria kutoka Mwanza hadi Bukoba mkoani Kagera.

aeneo aliyokagua kwenye meli hiyo ni pamoja na vyumba vya abiria vikiwemo vyumba maalumu kwa ajili ya huduma za mama na mtoto, chumba cha kuongozea meli, migahawa na chumba cha injini.

“Nimeona ukarabati mkubwa uliofanywa, nimeona injini mpya, meli imekamilika na ilishafanyiwa majaribio ya aina zote kubeba abiria na kubeba mizigo na wataalamu wamejiridhisha kuwa ina uwezo wa kubeba abiria na mizigo.”alisema Majaliwa.

“Haya yote ni mawazo na mipango ya Rais Dk John Magufuli pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015-2020. Tumetekeleza na tunaendelea kutekeleza.”alisema.

Baada ya kuikagua meli hiyo Majaliwa alikagua ujenzi wa chelezo na meli mpya na alieleza kuwa amerid hishwa na kazi inayoendelea kufanyika na akatoa wito kwa Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali.

Awali, Meneja Miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Luteni Kanali Vitus Mapunda alisema ukarabati wa meli ya MV New Victoria Hapa Kazi Tu yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tano 400 umegharimu sh. 22,712,098,200. Meli hiyo itatoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Mwanza Kaskazini, Kemondo na Bukoba.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi