loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maalim Seif aahidi kukubali matokeo

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amesema akishindwa katika Uchaguzi Mkuu ataheshimu matokeo na ameahidi kufanya kampeni kwa amani, utulivu na kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar.

Amewaeleza waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Vuga mjini Unguja kuwa, chama hicho kitafanya kampeni kistaarabu na ametoa wito kwa vyama vingine viheshimu sheria za uchaguzi.

Alisema Wazanzibari wanahitaji chama kitakachowaunganisha na kwamba, yeye amedhamiria kuifanya kazi hiyo kama akichaguliwa na kupewa ridhaa ya wananchi kushika dola.

“Nikishindwa katika uchaguzi mkuu nitaheshimu matokeo yatakayotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC...lakini namtaka mgombea mwenzangu wa Chama Cha Mapinduzi naye atoe tamko kama hili ili kuhakikisha kwamba Uchaguzi Mkuu unafanyika katika mazingira ya kidemokrasia na kupunguza joto la kisiasa”alisema Hamad.

Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi na kutoa nafasi kwa wafuasi wa chama hicho kushiriki katika mapokezi ya viongozi wao katika Bandari ya Malindi.

“Tupo tayari kufanya kazi na Jeshi la Polisi katika kulinda amani na utulivu...jeshi limetupa imani kubwa kwamba uchaguzi wetu utafanyika katika mazingira ya kuheshimu vyama vya siasa”alisema Hamad.

Mapema mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho Bernard Membe alisema amejiunga na ACT Wazalendo kwa matarajio ya kudumisha demokrasia ya vyama vingi na hajatumwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenda kuvuruga vyama vya upinzani.

Alisema yeye amefukuzwa CCM na amejiunga na ACT-Wazalendo kwenda kuimarisha nguvu ya upinzani na kamwe asifananishwe na mawaziri wakuu wastaafu waliojiunga na chama hicho kwa tamaa ya kupata uongozi.

”Nimejiunga na ACT-Wazalendo kwa ajili ya kuimarisha demokrasia katika mfumo wa vyama vingi... wenzangu na mawaziri wakuu wastaafu wamerudi kwa ajili ya kulinda marupurupu yao”alisema Memba.

MGOMBEA Urais kwa tiketi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi