loader
Kamala ateuliwa mgombea mwenza wa Biden

Kamala ateuliwa mgombea mwenza wa Biden

MGOMBEA urais wa chama cha Democratic, Joel Biden amemteua Kamala Harris kuwa mgombea mwenza, ikiwa ni mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi mwenye asili ya Asia kugombea nafasi hiyo.

Mwanamama huyo ambaye ni Seneta wa California, mwenye asili ya India na Jamaica, aliwahi kuwa hasimu wa Biden katika mchuano wa kuwania urais. Seneta huyo amekuwa akichukuliwa kwa muda mrefu kama mgombea wa nafasi ya pili baada ya Biden.

Mara kadhaa mwanasheria huyo mkuu wa zamani wa California aliwahi kutoa mwito wa kufanyika kwa mageuzi katika Idara ya Polisi ya Marekani wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Biden atachuana na mgombea wa chama cha Republican, Rais Donald Trump katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 3, mwaka huu.

Kamala alisema kuwa wakati wote amekuwa akijivunia utambulisho wake kama mwanamke mweusi na anajitambua binafsi kuwa ni Mmarekani

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/87200e9428103964356ae2cc4d229cea.JPG

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON DC, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi