loader
Kivumbi Ligi ya Mabingwa Ulaya

Kivumbi Ligi ya Mabingwa Ulaya

S IKU 414 baada kuanza kwa msimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019/20 huku Feronikeli ya Kosovo ikiichapa Lincoln Red Imps ya Gibraltar katika hatua ya awali ya kufuzu ya michuano hiyo, mechi za michuano hiyo zimerejea tena.

Katika hatua ya mtoano ya robo fainali hadi tamati ya mashindano hayo, kutakuwa na siku kama 12 za mtifuano jijini Lisbon kabla ya bingwa kukabidhiwa taji hilo ambalo hadi sasa halina mwenyewe baada ya Liverpool kuondolewa. B

aada ya Liverpool kuondolewa na Atletico Madrid tangu Machi, timu hiyo ilitamba nyumbani baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya England ikiwaacha Manchester City wakiutafuta ubingwa huo kwa tochi bila mafanikio.

TIMU ZILIZOBAKI

Mechi za robo fainali hadi fainali zitachezwa jijini Lisbon kwenye viwanja viwili tofauti na ilivyokuwa awali, mechi za michuano hiyo zilipokuwa zikichezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini.

Ligi ya Mabingwa Ukaya kama ilivyo kwa michuano mingine mikubwa barani humo, ilisimamishwa tangu Machi kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona. Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) liliamua tangu Juni kuwa jiji la Lisbon nchini Ureno ndio liandae mechi hizo kuanzia hatua ya robo fainali kutokana na miundombinu yake, ambapo vitatumika viwanja viwili vitakavyoshirikisha timu nane.

TIMU SHIRIKI

Timu nane zilizofuzu kucheza hatua ya robo fainali iliyoanza jana Jumatano usiku ni Atalanta, Paris St-Germain (PSG), RB Leipzig, Atletico Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester City na Lyon.

Ufaransa imeingiza timu mbili, PSG na Lyon, huku Ujerumani nayo ikiwa na timu mbili za Bayern Munich na RB Leipzig, wakati Hispania nayo ina timu mbili za Atletico Madrid na Barcelona na Italia ina timu moja ya Atalanta, huku England ikiwa na timu moja ya Man City.

Timu ngeni ya Atalanta jana usiku ilitarajiwa kupepetana na kikosi cha Paris Saint-Germain kinachoongozwa na Mbrazil Neymar. RATIBA KAMILI Viwanja vinavyotarajia kutumika ni cha michezo cha Jose Alvalade na cha Benfica cha Luz.

Kati ya timu zote zilifuzu kwa hatua ya robo fainali, ni mbili tu za Barcelona na Bayern Munich zilizowahi kutwaa mataji ya Ulaya, ambapo zote zimewahi kutwaa mara tano na zitakuna Ijumaa katika hatua hiyo na katika mpambano huo lazima mmoja atoke.

Atletico Madrid imewahi mara mbili kucheza fainali katika kipindi cha miaka saba iliyopita, lakini nusu fainali kampeni nzuri itakuwa kwa Paris StGermain, Manchester City na Lyon.

RB Leipzig haijawahi kuvuka hatua ya makundi kabla ya mwaka huu kufanya hivyo, wakati Atalanta huu ni msimu wake wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo itajaribu kupambana kufa au kupona ili ifanye vizuri.

LEO ALHAMISI

Timu ya RB Leipzig itakutana na Atletico Madrid katika mchezo wa pili wa robo fainali utakaopigwa leo. Hata hivyo, RB Leipzig itamkosa mkali wake wa mabao, Timo Werner, baada ya mchezaji huyo kusajiliwa na Chelsea kwa kiasi cha pauni milioni 54.

Werner alifunga mabao 34 katika mashindano yote wakati kikosi cha kocha Julian Nagelsmann kikimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani ya Bundesliga na kukosekana kwake kutakuwa hasara kubwa.

MECHI YA IJUMAA

Vinara Barcelona watakutana na Bayern Munich kesho Ijumaa, ambapo timu hizo zina rekodi sawa baada ya kila moja kutwaa mara tano taji hilo la Ulaya. Barca msimu huu haiko katika ubora wake, ambapo ilipoteza taji la La Liga kwa Real Madrid na kibarua cha kocha Quique Setien kipo katika hati hati, lakini inajivunia uwepo wa Lionel Messi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alifunga bao jingine la ajabu na kuiondoa Napoli katika hatua ya 16 bora. Bayern Munich kwa sasa ndio inasemekana kuwa timu bora kabisa barani Ulaya msimu huu.

Katika kudhihirisha ubora wake, Bayern Munich iliisambaratisha Chelsea kwa jumla ya mabao 7-1 na ina nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo huko Lisbon.

MECHI YA JUMAMOSI

Manchester City itakwaana na Lyon katika robo fainali nyingine itakayofanyika Jumamosi. Ni miaka minne sasa tangu timu hiyo ilipocheza nusu fainali na kwa sasa ndio inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo na kucheza nusu fainali baada ya kuichapa Real Madrid katika mechi za mikondo miwili.

Hata hivyo, Man City inatakiwa kuwa makini katika mchezo huo, kwani Lyon wako vizuri na lolote linaweza kutokea. Sergio Aguero ni nyota mwingine ambaye atakosa mchezo huo kutokana na majeruhi, lakini Gabriel Jesus alifanya kweli dhidi ya Real na kwa City kufunga mabao sio tatizo msimu huu.

Ni miaka tisa sasa tangu kocha Pep Guardiola alipotwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Je, msimu huu atafanya hivyo tena?

MESS PASUA KICHWA

Kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, amesema vigogo hao wa Ujerumani wanafanyia kazi jinsi ya kumzuia mchezaji nyota wa Barcelona mwenye kipaji, Lionel Messi kuelekea mchezo huo wa Ijumaa.

“Maelfu ya watu kabla yangu walijaribu kujibu swali hili. Hilo litawezekana kwa kucheza kwa pamoja,” alisema Goretzka wakati akijibu swali la waandishi wa habari juzi jijini Lisbon wakati alipoulizwa jinsi ya kumzuia Messi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/70ae4fc149f2799494f12f2853ba9cb5.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: NYON, Uswisi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi