loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha wa Barcelona atua Yanga

IMEBAINIKA muda wowote Klabu ya Yanga itamtambulisha Kaze Cedric raia wa Burundi kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo baada ya mazungumzo ya pande mbili kuonekana kufika sehemu nzuri.

Cedric anayeishi Canada kwa sasa ni mmoja kati ya makocha waliopo kwenye programu ya makocha wa Klabu ya FC Barcelona ya Hispania kwa miaka mingi.

Licha ya kuwa ni kocha mwenye uwezo mkubwa, hasa katika kuibua vipaji na kuviendeleza, Cedric aliyekuwa akicheza nafasi ya ulinzi hakupata mafanikio makubwa kwenye maisha yake ya kucheza soka, ikiwemo kutoichezea timu ya taifa ya Burundi.

Yanga iliyoingia kambini jana ikiwa chini ya kocha msaidizi Riedoh Berdien mpaka sasa haina Kocha Mkuu baada ya kumfuta kazi Luc Eymael mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi karibuni.

Yanga itakuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Shule ya Sheria uliopo Ubungo Mawasiliano, Dar es Salaam.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa mpango ya kumchukua kocha Florent Ibenge wa AS Vita Club imeshasitishwa na muda wowote Mrundi huyo atatangazwa kuziba nafasi iliyoachwa na Eymael.

Taarifa hizo ziliendelea kusema uongozi umeamua kumchukua kocha huyo wakimuamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kuijenga timu kutokana na kufanya kazi na Barcelona kwa muda mrefu. 

Gazeti hili lilimtafuta Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuelezea taarifa hizo kwa kina alisema hawezi kuweka wazi kila kitu kutokana na mchakato wa kumtafuta kocha bado haujakamilika.

Alisema kuwa Yanga imekuwa na kawaida ya kuweka wazi mambo yake mara tu yanapokamilika, hivyo anachoweza kusema kwa sasa ni kwamba mchakato wa kumpata kocha mpya unaendelea na utakamilika hivi karibuni.

“Siwezi kusema tulipofikia wala kumtaja tunayemtaka ila Wanayanga watambue tunaendelea na mchakato wa kumpata kocha wetu mpya, tukisha kamilisha basi watamjua hatutaweza kuwaficha,” alisema Bumbuli.

TIMU ya KMC iliendeleza ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi