loader
Shule zasubiri tamko la Museveni kufunguliwa

Shule zasubiri tamko la Museveni kufunguliwa

WIZARA za afya na elimu ya juu, zimesema hatma ya shule kufunguliwa au kutofungulia mwaka huu ipo kwa Rais wa Yoweri Museveni.

Katika taarifa ya pamoja kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda, wizara hizo zimeeleza hali halisi ilivyo mpaka sasa na kwamba uamuzi wa kufunguliwa au kutofunguliwa shule unasubiri kauli ya Rais Museveni.

Waziri wa Elimu ya Juu, Dk John Muyingo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, maelezo yote pamoja na mapendekezo wamempelekea Rais Museveni ilia toe maamuzi ya mwisho kuhusu kufunguliwa au kutofunguliwa kwa shule.

“Sasa hivi tunamsubiri Rais atoe maamuzi, kwa sababu yeye ndio mwenye mamlaka ya kufunga na kufungua shule. Tumempatia taarifa zote muhimu kuhusu maambukizi ya corona pamoja na hali halisi ilivyo kwa sasa,” alisema Muyingo.

Waziri wa Afya, Dk Jane Aceng, alisema wizara zote mbili pamoja na kikosi kazi cha kupambana na corona, wametengeneza muongozo wa namna wanafunzi na walimu wanaweza kuwa salama endapo shule zitafunguliwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e9e65f040857f6dbbeb94ea47266ff08.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments