loader
Kanisa lililoharibiwa kujengwa upya

Kanisa lililoharibiwa kujengwa upya

SERIKALI imesema italijenga upya Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko Ndeeba, ambalo hivi karibuni liliharibiwa kabisa kutokana na mgogoro wa miaka zaidi ya arobaini iliyopita.

Rais Yoweri Museveni alitoa ahadi hiyo alipotembelea eneo juzi kujionea uharibifu uliofanywa, ambapo kanisa hilo lililojenga miaka mingi iliyopita liliharibiwa kabisa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais Museveni alifanya ziara ya ghafla katika eneo hilo, ambapo alilaani kitendo hicho na kukielezea kuwa kinaweza kufanywa na mtu ambaye hana hofu ya Mungu.

“Kitendo cha kijinga kama hiki kilichofanywa katika kanisa hili kinaweza tu kufanywa na watu ambao hawana heshina na mahala patakatifu na hawamwogopi Muumba wao.” 

“Nawaahidi kuwa, kanisa hili litajengwa lote na serikali,” alisema na kuibua furaha kwa watu waliokuwepo katika eneo hilo.

Rais Museveni alisema mtu aliyebomoa kanisa hilo ni mtumishi wa serikali, ambaye ana utajiri, lakini anautumia vibaya.

Kiongozi wa kanisa hilo, Augustine Kayemba, alimshukuru Rais Museveni kwa ahadi hiyo aliyosema imepokewa kwa unyenyekevu na waamini wote pamoja na Wakristo wote wa Uganda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1fa1c1cc0a1e12d160bf6a581fa40bbe.jpeg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi