loader
Michelle Obama  amshambulia Trump

Michelle Obama amshambulia Trump

MICHELLE Obama amemshambulia kwa maneno Rais wa Marekani, Donald Trump wakati chama cha Democrats kimeanza rasmi kampeni yake ambapo Joe Biden ndiye mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba, mwaka huu.

"Donald Trump si rais sahihi kwa nchi yetu," alisema Michelle, ambaye ni  mke wa Rais mstaafu Barack Obama. Alisema hayo katika ujumbe wake uliorekodiwa wakati wa mkutano wa chama cha Democrats.

Waasi wa chama cha Trump cha Republican, pia nao hawakusita kutoa yaliyo moyoni wakati wa mkutano huo.

Kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona, Democrats ilifuta mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika na shughuli nyingine zote za kisiasa huko, Milwaukee, Wisconsin.

Lakini haijafahamika ikiwa mikutano hiyo kwa njia ya mtandao ambayo hotuba zake zimerekodiwa na bila uwepo wa watu wanaoshuhudia moja kwa moja kunaweza kusababisha msisimko ule kama ya wakati wa kabla ya janga la corona.

Chama cha Republican kitakumbana na changamoto hiyo wakati wanathibitishia umma umuhimu wao wa kuwa uongozini katika kipindi cha miaka minne kwenye mkutano wao uliopangwa kufanyika wiki ijayo.

Mke huyo wa Obama ambaye hotuba yake ilirekodiwa kabla ya Biden kutangaza mgombea mwenza, Seneta Kamala Harris, siku sita zilizopita, alianza kwa kumshambulia Trump kwa maneno.

"Huwezi kudanganya mienendo yako unapofanya kazi," alisema hivyo kwenye hotuba yake ambayo ilifunga siku ya kwanza ya mkutano wa chama cha Democrats.

Msemaji huyo mkuu wa siku aliongeza: "Uchumi wetu unadidimia kwa sababu ya virusi ambavyo huyu rais alivipuuza kwa muda mrefu."

"Kusema ukweli ulio wazi kwamba maisha ya mtu mweusi ni muhimu bado ni jambo linalofanyiwa dhihaka katika ofisi ya juu," alisisitiza

Alisema kila wamarekani wanapogeukia Ikulu kwa uongozi, au kutaka kupata faraja au kupata nguvu ya uimara, badala yake wanachopata ni ghasia, mgawanyiko na ukosefu wa uelewa.

Alisema miaka minne iliyopita imekuwa na changamoto nyingi kujieleza kwa watoto wa Marekani. "Wanaona viongozi wetu wakiitwa wengine maadui wa serikali na kuhamasisha dhana ya kuwa mtu mweupe ni bora.”.

"Wanaangalia kwa hofu wakati watoto wanapotenganishwa na familia wanapotupwa kizimbani, kurushiwa maji ya kuwasha na mabomu ya rashasha yanatumiwa katika maandamano ya amani kwa sababu tu ya nafasi ya kutaka kupiga picha," alisema.

Alisema Trump alikuwa rais stahiki wa taifa hilo, lakini amekuwa na wakati mgumu kujidhihirisha kwamba anaweza kufanya kazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/be9e9a4166985dbf1c01f544744e9ce3.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi