loader
WHO, UNICEF zataka shule zifunguliwe barani Afrika

WHO, UNICEF zataka shule zifunguliwe barani Afrika

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Watoto (Unicef), yametaka serikali za Afrika kufungua shule zenye mazingira salama wakati huu wa janga la corona.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kuna madhara kwa wanafunzi.

Kutokana hali hiyo, mashirika hayo sasa yanazitaka serikali kuwekeza katika huduma za usafi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona katika taasisi za masomo.

Mashirika hayo mawili yalisema kuwa wanafunzi wanawekwa katika hatari ya lishe duni, mimba za utotoni na ghasia wakati huu wa kurefushwa kwa muda wa kukaa nyumbani.

Shule katika nchi za Afrika ni mahali salama kwa watoto, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa WHO, Matshidiso Moeti.

“Hatupaswi kusahau juhudi zetu za kudhibiti Covid-19. Wakati nchi zinafungua shughuli za kila siku kwa kuzingatia usalama, tunaweza kufungua tena shule,” alisema Moeti katika mkutano wa video jana. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Unicef wa Kanda, Mohamed Fall alisema kufungwa kwa muda mrefu kwa shule, kunaathiri maisha ya baadaye ya watoto na jamii.

Ni nchi sita tu za Afrika ambazo zimefungua kikamilifu shule na hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na WHO na Unicef katika nchi 39.

Katika baadhi ya nchi shule zilifunguliwa na baadaye kufungwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Nyingine zinafungua shule kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa ajili ya kufanya mitihani muhimu. Nchi kama Kenya zimefuta mwaka wa masomo wa 2020

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c769e0ec2ea8ab4792a731f3b47310ca.jpg

MWANAMIELEKA na Muigizaji Maarufu Dwayne Johnson ...

foto
Mwandishi: GENEVA, Uswisi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi