loader
Biden aapa kuumaliza utawala wa Trump

Biden aapa kuumaliza utawala wa Trump

MGOMBEA urais wa chama cha Democrats katika ngazi ya kuwania urais nchini Marekani, Joe Biden (77)  amesema Rais aliyepo madarakani na mpinzani wake kwenye uchaguzi, Donald Trump, ameiweka nchi hiyo gizani kwa muda mrefu.

Biden aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo, alisema uongozi wa Trump umeibua hasira nyingi, uoga na kuwagawa Wamerekani.

Mgombea huyo atakabiliana na Trump akiwa anaongoza kwenye kura za maoni dhidi ya mpinzani wake huyo.

Lakini zikiwa zimebaki siku 75 ili kufikia siku ya kupiga kura, bado Rais Trump wa chama cha Republican, ana nafasi ya kuziba pengo hilo kwenye kura hizo za maoni.

Biden alikuwa akizungumza katika mkutano wa mwisho wa mfululizo wa mikutano ya Democrats.

Katika mikutano hiyo yote, hakukuwa na shamrashamra, shangwe na mabango na wanachama kutokana na janga la ugonjwa wa corona.

Waandaaji wa mikutano hiyo walitumia zaidi hotuba za viongozi wa chama hicho, zilizorekodiwa na kusikilizishwa kwa wanachama.

Akizungumza akiwa nyumbani kwake Wilmington huko Delaware, Biden alisema “Nawaahidi leo mbele yenu kuwa mkinipa fursa ya kuwa rais wenu nitahakikisha natumia kila kilicho kizuri chetu na si kibaya chetu, nitakuwa mshirika wenu katika mwanga na si katika giza,”

“Tukiwa tumeungana tutakikabili hiki kipindi cha giza hapa Marekani. Tutachagua matumaini dhidi ya hofu, ukweli dhidi ya nadharia, usawa dhidi ya upendeleo,” alisema

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/877253fe2b0eb488d5f486ab8429bced.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi