loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kiwanja cha kubeba mashabiki 15,000 kujenga Geita

Kiwanja cha kubeba mashabiki 15,000 kujenga Geita

MKOA  wa Geita umeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu utakaokuwa na uwezo wa kubeba  mashabiki 15,000 kwa wakati mmoja ili kuondoa changamoto za viwanja kwa mikoa ya kanda ya ziwa.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema tayari mkandarasi Shirika la Uzalisha Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), wameshaanza baadhi ya matengenezi.

“Wameanza kuchimba udongo na kurekebisha eneo la uwanja la kuchezea ili kuliweka sawa. Na baada ya hapo wataliangalia eneo la majukwaa ya uwanja huo kwa kuweka paa,” anasema Gabriel

Mkuu huyo wa mkoa amesema uwanja huo utajengwa kwa awamu kwa kutegemea vyanzo vya mapato ya ndani unatarajiwa kuchukua miaka minne kukamilika.

 “Uwepo wa uwanja utasaidia kuvutia wawekezaji na pia kukuza vipaji vya vijana wa mkoa wa Geita lakini pia kukuza sekta ya michezo mkoa wa Geita,” amesema Mhandisi Gabriel.

Hata hivyo uwanja huo utakapokamilika unatajwa kuwa chachu ya kupata timu shiriki kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5d491e2a13830fd3b3dec6df997bc015.jpg

MSANII wa Bongo Movie  ambaye pia ni ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi