loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi: Nitaijenga Zanzibar kwa kasi mpya

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Ali Mwinyi Dk Mwinyi amesema ataendeleza atakapofikia Rais Mohamed Shein kwa kasi mpya na kwa nguvu ya kutosha.

Amesisitiza kwamba  Watanzania wapo tayari kumchagua yeye,  Rais John Magufuli na wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani.

Kwa upande wake, Rais Shein amesema  Dk Ali Mwinyi ni mzalendo halisi  na kwamba Wazanzibari wanasubiri wakati ufike wamchague kwa kishindo kikubwa.

Hayo yalisemwa jana kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM,  uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, ambao pamoja na masuala mengine, Dk Shein alimtambulisha Dk Mwinyi kwa wananchi. 

"Sisi tuliopo Zanzibar tutahakikisha kwamba Mwinyi anashinda kuwa Rais wa Zanzibar. Kama mimi nilivyochaguliwa wakati ule kule Zanzibar kwa misingi na heshima ileile," alisema Rais Shein  na kumsifia namna anavyotekeleza kikamilifu kazi zake alizopewa katika Serikali ya Muungano. 

Alisema Watanzania waliofurika ndani  na nje ya uwanja huo,  wanafahamu Dk Mwinyi ambaye amekuwa mtendaji mwenye weledi kwa kila kazi aliyopewa. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya, Waziri wa Afya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na  Waziri wa Ulinzi; wadhifa anaoendelea nao hadi sasa. 

"Jina lake ni maarufu miongoni mwetu, ni kiongozi mwenzetu, ni kiongozi halisi wa CCM, ana sifa zote za uongozi kwenye chama chetu na lakini vilevile anasifa za kuwa Rais wa Zanzibar baadaye," alisema Dk Shein.

Alisema kutokana na sifa hizo, ndiyo maana Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ilimchagulia kuwa mgombea nafasi ya Rais kwa Zanzibar ili CCM iendelee kuongoza Zanzibar . 

Alisema Dk Mwinyi ana uwezo mkubwa na kitaaluma ni daktari mbobevu katika magonjwa ya ndani ya binadamu. "Ana heshima kubwa ndani na nje ya nchi, anatambulika kwa sifa zake binafsi, sifa hizo ndizo zlizofanya CCM kumchagua kugombea urais wa Zanazibar.

"Dk Mwinyi ni mzalendo halisi sana, kazi zote alizokabidhiwa na Serikali ya Muungano amezifanya kwa ufanisi mkubwa sana," alisema.

Dk Shein alisema anaamini kama wengine wanavyoamini kwamba Dk Mwinyi atawavusha katika nafasi ya urais Zanzibar na CCM itaibuka kidedea na kupata ushindi. Anaamini ndani ya nafsi yake na pia wenzake wana CCM wanaamini katika nafsi kwamba atashinda.

Alisema wanapozindua Kampeni na Ilani ya 2020-2025, wanaCCM wanatakiwa kuendelea kuchagua viongozi wa CCM akiwamo Rais wa Muungano Rais John Magufuli awe rais na kwamba watakuwa pia wamechagua Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wake. 

Kwa upande wake, Dk Mwinyi alisema ataendeleza atakapofikia Rais Shein kwa  kasi mpya,  zaidi na kwa nguvu ya kutosha.

Aliahidi kuendeleza kazi zuri zilizoanzishwa na Rais Shein, akisisitiza kwamba amefanya mambo mengi ya maendeleo kuanzia kwenye huduma za jamii na miundombinu na katika sekta nyingine. “Tutaenda kwa spidi mpya, kwa kasi zaidi kwa nguvu ya kutosha," alisema.

Dk Mwinyi alisema hana shaka kwa upande wa Tanzania Bara, kazi aliyoanza Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano, wote wameona na kama atapewa kipindi cha pili sijui watasemaje.  

Aliwakumbusha wana CCM kutobweteka, bali wajitokeze kwa wingi Oktoba 28 kwenda kupira kura  kuchagua viongozi wote wa CCM katika maeneo yote. 

Aliwataka wana-CCM kulinda amani waliyokuwa nayo kwa kusema, bila amani hakuna maendeleo. Alisema, wana CCM Zanzibar wapo tayari kuwachagua viongozi wa CCM katika ngazi zote.

"Wapo tayari kumchagua Rais wa Muungano John Magufuli, Rais wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani, kwa hivyo tunachosubiri kule ni siku ya uchaguzi, nadhani kazi imeshaandaliwa".

Pia alishukuru Rais Dk Shein kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Zanzibar, kazi yao mwaka huu imekuwa nyepesi kama wanavyotambua kwamba pande zote mbili ilani ya uchaguzi imetekelezwa vizuri.

Alisema Tanzania Bara hakuna haja kuyasema kwani Rais Magufuli amefanya mengi, lakini kule Zanzibar pia yametekelezwa mazuri mengi, hivyo hiyo itasaidia kupita kwa kishindo na hilo hana shaka nalo.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi