loader
UAE yafuta sheria ya kuisusia Israel

UAE yafuta sheria ya kuisusia Israel

RAIS wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Khalifa bin Zayed Al Nahyan ametoa amri ya kufuta sheria ya kuisusia Israeli na kuruhusu mikataba ya biashara na fedha kati ya nchi hizo mbili.

Amri hiyo ya kiutendaji kutoka kwa Nahyan inalenga kuunga mkono ushirikiano wa pande mbili kwa ajili ya kufikia uhusiano kati ya nchi hizo.

Amri hiyo imetolewa wakati shirika la ndege la Israel, El Al, likipanga kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv na mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi.

Ndege ya shirika hilo itakuwa na ujumbe wa ngazi ya juu wa Israel na wasaidizi wa ngazi ya juu wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwenda leo UEA. Trump alisimamia makubaliano ya kurudisha uhusiano kati ya Israeli na UAE Agosti 13, mwaka huu.

Mshauri wa ngazi ya juu wa Trump, Jared Kushner atakuwa mmoja wa maofisa wa Marekani katika ndege hiyo ya El Al, itakayoanza safari yake leo saa 4 asubuhi.

Makubaliano kati ya Israel naUAE, yanasubiri mazungumzo kuhusu maelezo ya namna ya kufungua balozi baina yao, biashara na muungano wa safari.  Yatakapomilika ndipo makubaliano rasmi yatasainiwa rasmi.

Hakuna safari za ndege kati ya Israeli na UAE. Haijawekwa wazi pia iwapo El Al itaweza kurusha ndege yake katika anga ya Saudi Arabia, ambayo haina uhusiano rasmi na Israeli. Saudi Arabia ikikubali itapunguza muda wa safari hiyo.

Mei mwaka huu ndege ya shirika la ndege la Etihad, ilifanya safari kutoka UAE kwenda Tel Aviv kupeleka mahitaji kwa Wapalestina kwa ajili ya kutumika katika janga la virusi vya corona. Hiyo ilikuwa safari ya kwanza inayojulikana, iliyofanywa na ndege ya UAE kwenda Israeli.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/26340a5035ad3169b87a79a45e8a564c.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: ABU DHABI, UAE

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi