loader
Wauza mitumba  watakiwa kujisajili

Wauza mitumba watakiwa kujisajili

BAADA ya serikali kurejesha uingizaji mitumba nchini, wafanyabiashara wa nguo hizo wametakiwa kujisajili katika Shirika la Viwango Kenya na kupatiwa cheti maalumu.

Hatua hiyo ni sehemu ya utaratibu wa serikali kupunguza vikwazo vya kibiashara na huduma nyingine, ikiwamo kuondoa zuio la uingizaji mitumba.

Katika mkutano baina ya Rais Rais Uhuru Kenyatta na wawakilishi wa Chama cha Waagizaji Mitumba Kenya chini ya Mwenyekiti wao, Teresia Njenga, wamekubaliana nguo hizo kufungashwa katika marobota yasiyozidi kilo 50.

Taarifa ya msemaji wa Ikulu, Kanze Dena, ilieleza kuwa, pande hizo mbili zimekubaliana nguo za mitumba kabla ya kusafirishwa kupuliziwa dawa ili kwenda sambamba na matakwa ya Wizara ya Afya, Wizara ya Viwanda na Shirika la Viwango Kenya.

Pia katika kurahisisha ukaguzi na kodi, wafanyabiashara wa jumla wa mitumba wanatakiwa kuwasilisha kwa Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) na KEBS orodha ya wanunuzi wao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8ed35ec089ffc5324f7200619200c658.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi