loader
Serikali yapokea dawa za malaria sugu

Serikali yapokea dawa za malaria sugu

WAZIRI wa Afya amepokea dawa za kuzuia ugonjwa wa malaria zenye thamani ya Sh milioni 73 zenye uwezo wa kutibu wagonjwa 70,000 wenye malaria kali.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Rashid Aman, alisema dawa hizo zimetolewa na kampuni ya Fosun Pharma ya China, ikiwamo za sindano za artesunate za kutibu malaria kali.

Alisema sindano zilizotolewa ni 400,000 zenye thamani ya takribani Sh milioni 73 ambazo zina uwezo wa kutibu wagonjwa 70,000 wenye malaria kali.

Mwaka jana wagonjwa 250,000 wa malaria kali walitibiwa na dawa za artesunate katika sekta za umma, huku asilimia 75 wakiwa watoto chini ya miaka 15.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2c7fd6ee81a3509cc8335cf3207ae099.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi