loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sholo Mwamba: Singeli ibadilike

MSANII wa muziki wa gingeli, Sholo Mwamba amesema singeli imepata nafasi mbele ya Rais sasa inabidi ibadilike.

Sholo Mwamba ametoa kauli hiyo  baada ya kutoa burudani katika kampeni ya mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli mkoani Shinyanga na kusimama na kucheza wimbo huo.

 "Kikubwa ni kumshukru Mungu kwa sababu sijategemea kama ingekuwa vile, kwa uwezo wa Mungu ameamua kunibariki kijana wake, nilishawahi kuota kwenye ndoto zangu siku moja nitaimba halafu Rais atacheza,"

"Baada ya pale nilizungumza na Rais Magufuli kupitia simu ya Ikulu Mawasiliano kwa Gerson Msigwa na amesema amependa nilichofanya na nilivyovaa kitamaduni, pia ametusihi kuongeza ubunifu. 

"Tangu nilivyomaliza kutumbuiza pale nimeshindwa kulala mpaka sasa hivi, yaani siamini kama ni mimi kweli ambaye Rais amecheza wimbo wangu, kikubwa zaidi namshukuru Mungu na mashabiki wetu waendelee kusapoti muziki wa singeli," alimaliza.

WANAWAKE wamekuwa ni chachu kubwa ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi