loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mjasiriamali aliyekataa vikwazo kuzima ndoto zake

HAPA Tanzania kuna watu wana ndoto kubwa ambazo zinaweza kuifanya nchi kuonekana kwenye mataifa mbalimbali endapo watapewa nafasi na kuwezeshwa.

Mwanamke mjasiriamali, Agatha Laizer anayesindika siagi ya karanga ‘peanut butter’, anasema hayo wakati akielezea safari yake ya mafanikio na vikwazo alivyokumbana navyo katika ujasiriamali.

Anasema anamshukuru Mungu kufikia hapo alipo kutokana na historia aliyoipitia huko nyuma, ambayo imekuwa ni njia nzuri ya kumfundisha jinsi ya kusimama na kujitegemea kama mjasiriamali na kuwa sehemu ya kusaidia familia yake.

Agatha anasema anajitahidi kusindika karanga kwa kutumia ubunifu wa aina mbalimbali ambao unafanya bidhaa hiyo ya karanga iweze kuonekana tofauti.

Pia anaeleza kuwa anajitahidi kufanya kazi na wakulima wa karanga pamoja na wajasiriamali wadogo wanaoweza kuuza bidhaa yake ili nao waweze kubadilisha maisha yao.

Kwa maelezo ya mjasiriamali huyo, miaka ya nyuma aliwahi kufanya kazi za kuajiriwa alipomaliza chuo, yakiwemo masuala ya utalii katika Hoteli ya Serena, meneja uhusiano kwenye kampuni ya utalii, baadaye alianza kujiajiri baada ya mume wake kumfungulia duka la jumla la mahitaji ya nyumbani.

Anasema alifanya biashara hiyo ya duka la jumla alilofunguliwa na mume wake Tuheri Thobias, lakini kwa kuwa alikuwa na hali ya ubunifu aliendelea kujiongeza kama mjasiriamali kwa kufanya kitu kinachoonekana na kinachogusa jamii.

“Basi baada ya kuwa na duka hilo, sikuona kama ni kitu ninachopenda kukifanya, nikajiongeza nikafungua duka la ubunifu wa mavazi, nikawa nashona nguo, mapazia mpaka mazulia, kazi ambayo niliifanya nikawa na jina sana na nilikuwa napenda nikimbunia mtu mmoja asifanane na mwingine,” anasema.

Hata hivyo, kazi hiyo ya ubunifu haikufika mbali kwa kuwa wateja wengi walikuwa hawalipi kwa wakati, jambo lililomrudisha nyuma.

Agatha anasema anamshukuru sana mama yake Sara Kessy ambaye aliona maono ndani yake kisha kumshawishi mwaka 1997 ajiunge na Shule ya Usindikaji iliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) wakishirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo (Sido).

“Ni kazi niliyokuwa naiona kama ya watu wazima sana ambayo ilikuwa hainivutii, mama yangu mzazi alisimama kuhakikisha kwamba ninajifunza na ninaweza kupata kitu kwenye kozi hiyo iliyokuwa ya miezi mitatu, ili niweze kusimama na kunisaidia kwa kuwa tayari alikuwa ameshaanza kazi hizo za mikono,” anasema.

Agatha anasema mafunzo hayo yalimsaidia kwani aliendelea kujifunza usindikaji na kujiongeza kwenye nyanja mbalimbali, kwa kutengeneza mvinyo, unga, viungo, asali pamoja na siagi hiyo ya karanga.

Anajivunia hilo kwa sababu kwenye mambo ya chakula anaweza kufanya kitu tofauti na jamii ikatambua kuna mtu fulani amefanya kitu fulani.

Anasema kuhusu kazi yake ya ubunifu aliiendeleza na aliweza kusafiri kwenda nchi mbalimbali ikiwepo China ambapo kabla hajaanza kujishughulisha na nguo alifungua saluni ya Kiafrika kwa kuwa anapenda kufanya kazi za mikono.

Agatha anasema baadaye alitafuta kiwanda ambacho alifanya nacho kazi za nguo, ilifika wakati Wachina wakaanza kutumia ubunifu wake na kutolesha nguo wao, kwa hiyo akawa na akiba kubwa ambayo ilimpa shida sana kuiuza.

Pamoja na changamoto hiyo anasema hakuacha kazi ya ujasiriamali aliyokuwa anaifanya na mama yake nchini Tanzania.

“Baada ya kupata hasara ile ya mambo ya nguo nilikuwa nimekata tamaa nikajiona basi kwa sababu nilishapoteza muda mwingi na wateja wengi walishanijua kwa hilo la mambo ya nguo ambao walikuwa ni watu wa mataifa mbalimbali.

“Nilikuwa na deal na watu kutoka Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC), Nigeria, Ghana, Togo, Mali na Senegal, hao wote ni sehemu ambazo naweza kusema wamevaa nguo ambazo nimezibuni mimi ambazo nilikuwa natoa design nawapa wachina kiwandani wanatengeneza ninauza,” anasema.

Anaongeza kuwa, “lakini sasa baada ya Wachina kuja kunakili ubunifu wangu ilinirudisha nyuma sana nikakaa zaidi ya miezi sita sijafanya kazi, mzigo umekaa pale zaidi ya dola za Marekani 10,000 ambayo kwa miaka hiyo 2005 na 2006 ilikuwa ni fedha nyingi sana.

“Lakini namshukuru Mungu sana amenipa mume Tuheri Thobias muelewa alisimama na mimi akanitia moyo, akasema umeshakaa huko muda mrefu umeshajua njia, kazi gani ya kuweza kufanya huko ukirudi huku ni kama unarudi nyuma hebu jaribu kusimama tena angalia kichwa chako bado kinafikiri vizuri, kinafanya mambo vizuri, hebu jaribu kufikikiria kitu kingine.”

Kwa maelezo yake alivyobaki China akawa anafanya kazi za usambazaji wa jumla lakini pia alikuwa anafanya pamoja na kuendeleza bidhaa ambazo tayari aliziacha, mama yake akiwa anaziendeleza kwenye uzalishaji.

Anasema mpaka leo hii anafurahi kuona alivyopiga hatua na bidhaa ambayo inajulikana sokoni pia inagusa jamii ‘halisi products’ unga wa lishe na viungo. Kwa mujibu wa Agatha baada ya kuona amekwama kabisa aliamua kurudi Tanzania kuendeleza ujasiriamali wake kwa kushirikiana na mama yake.

Akiwa hapa nchini mama yake alimtia moyo kwa kumwambia kushindwa kwenye jambo moja si mwisho wa dunia hivyo anaweza kufanya vizuri zaidi. Anasema familia yake ilisimama naye pamoja na mume wake aliyejitoa kwa hali na mali kuhakikisha yeye (Agatha) mke wake anapata kile ambacho anatamani kukifanya.

Kwenye safari yake hiyo, mama yake mzazi alimuamini na kumpa moyo wa kusimama mwenyewe, mume wake (Thobias) akakubali kusimama naye na pia wifi yake Selina Letara anasema amekuwa chachu na msaada mkubwa sana katika maendeleo yake.

“Watu hawa wamenisapoti kwa hali na mali, muda, wao kunitia moyo, kifedha jinsi yoyote ambayo niliona ninakwama, ninahitaji msaada wao walikuwa wapo na mimi kuhakikisha kuwa ninafanikiwa leo kufikia malengo yangu haya ambayo tuna bidhaa mezani inaitwa Tobi peanut butter,” anasema.

“Tobi peanut butter ni siagi ambayo najivunia kama Mtanzania, maana sasa hivi Tanzania ikiulizwa kama wana mzalishaji wa siagi ya karanga au hata yakitokea maonesho kama ya SADC, Jumuiya ya Afrika Mashariki nina uhakika wa kuiwakilisha nchi yangu ya Tanzania na kuhakikisha kuwa tunakuwa tunatambulika kuwa tuna siagi bora Tanzania inayotokana na karanga za wakulima wetu,” anasema.

Agatha anasema hilo ndilo jambo kubwa alilokutana nalo kwenye safari yake ya kutimiza ndoto aliyonayo ambayo imemwezesha mpaka sasa kuwa na wafanyakazi 22 katika kiwanda chake kijulikanacho kama ‘Seasoning Palet’ cha kutengeneza siagi ya karanga kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mwanadada Agatha ni mwenyeji wa Kaskazini, kabila lake ni mchaga kutoka Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, aliyeolewa na Mmasai.

Walijaliwa watoto wanne kwa bahati mbaya mmoja alifariki wakabaki watatu, wa kike wawili na mwanamume mmoja. Safari yake ya mafanikio ilianza mwaka jana akiwa nchini Tanzania baada ya kupitia changamoto mbalimbali za kupoteza mitaji wakati akiwa anaishi nchini China kwa miaka 14 alipokuwa akifanya biashara mbalimbali.

Mjasiriamali huyo alisoma katika Shule ya Msingi Levolosi iliyopo Manispaa ya Arusha Mjini, kisha sekondari alisoma katika Shule ya Wasichana ya Msalato, iliyopo Dodoma.

Baada ya hapo alisoma Chuo cha Uhazili Hanns Seidel Foundation kilichopo Manispaa ya Arusha mjini, kisha alisomea masuala ya Usimamizi wa Hoteli katika chuo hicho hicho cha Hanns Seidel Foundation.

Kwa maelezo yake, Agatha anasema akiwa hafanyi shughuli zake za ujasirimali hupendelea sana kupika na kuoka.

“Nafurahia sana kubuni mapishi mapya kila wakati na ninapendelea sana kusikiliza muziki wa country,” anase

WANAWAKE wamekuwa ni chachu kubwa ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi