loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mayai huchangia afya ya nywele

MASKI ya mayai ni moja ya tiba yenye nguvu kwa nywele zenye afya. Ni chanzo kikubwa cha vitamini. Vitamini B1 (thiamin), B2 (riboflavin) na B5 (pantothenic acid) ni muhimu kama unataka nywele zenye afya, kwani huzifanya nywele kubadilika, nguvu na ustawi kwa ujumla.

Biotin au Vitamin B7 ni muhimu kwa kukuza nywele wakati folic acid (vitamin b inayopatikana kwenye mboga za majani, maini) husaidia kutoka mvi kabla ya wakati.

Ili kuvipata vyote hivi mayai yanaweza kuwa tiba ya pamoja ya kuzifanya nywele zako kuwa na afya. Tumia vyote kiini na ute mweupe. Kiini hufanya kazi ya kilainishi (moisturizer) kwa nywele kavu na pia chakula kikubwa cha nywele kutokana na virutubisho vilivyopo ndani yake.

Vile vile husaidia kubakisha mng’ao wa nywele kutokana na faida ya vilainishi vilivyomo ndani yake.

Vunja mayai mawili na kisha yapigepige vizuri katika bakuli.

Paka kwenye nywele na ngozi ya kichwa na kisha acha kwa dakika 10. Kisha osha nywele zako vizuri kwa maji kwa kutumia shampuu na conditioner yako.

KWA sasa nchi nzima ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi