loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa:Tumeandaa mazingira Watanzania wajikomboe

Majaliwa:Tumeandaa mazingira Watanzania wajikomboe

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha Watanzania kujikwamua kiuchumi wakiwemo wafanyabiashara wadogo.

Ameyasema hayo leo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kirima Juu wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika mkutano huo Majaliwa alimuombea kura mgombea wa urais kupitia CCM John Magufuli, mgombea ubunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi na wagombea udiwani.

"Nimekuja hapa kuwaomba sana kura yenu ya ndio kwa Rais Dk Magufuli kwani mkiwa sehemu ya Watanzania mnafahamu kazi kubwa ya kupeleka maendeleo aliyoifanya nchi nzima bila ya ubaguzi wa aina yoyote, tuhakikishe tunampigia kura nyingi ili akaendeleze kazi aliyoianza."alisema Majaliwa.

Alisema, Serikali ya CCM imejenga miradi mingi ya kimkakati ikiwemo ya afya, maji, elimu, umeme, barabara, viwanja vya ndege kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya Watanzania na imetengeneza fursa katika maeneo mbalimbali zilizowezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

Akizungumzia kuhusu miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mkuu amesema jumla ya sh. bilioni 2.1 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Uru Kyaseni, Uru Kusini na Okaoni pamoja na upanuzi na ukarabati wa zahanati za Kahe, Kilema, Kisao, Chemchemi, Mowo, Kitowo na Kituo cha Afya Shimbwe. 

Pia sh bilioni 12.2zilitolewa kwa ajili ya ununuzi wadawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Kuhusu elimu ya msingi bila malipo, Majaliwa amesema Serikali imetoa bilioni sh. 4.8 kwa ajili ya ukarabati, utawala, michezo, mitihani na posho kwa maofisa elimu kata na walimu wakuu katika shule za msingi 252 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

"Serikali imetoa shilingi bilioni 10.2 kwa ajili ya fidia ya ada, chakula kwa shule za bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wasShule katika shule za sekondari 59 kwenye halmashauri ya wilaya ya Moshi."alisema.

Amesema shilingi bilioni 1.6 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 18, matundu ya vyoo 109, bwalo moja, nyumba sita za walimu na jengo moja la utawala na ununuzi wa mashine ya kudurufu mitihani katika shule za msingi Maweni, Mahoma, Ngaroni na Saghana.

Majaliwa alisema, sh bilioni 7.3 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 26, matundu vyoo 45, maabara 14, mabweni sita na ujenzi wa nyumba za walimu katika shule za sekondari za Ashira, Umbwe, Sakayo Mosha na Muungano, Kisarika, Shimbwe na Kimochi.

Alisema Serikali imetoa sh bilioni 5.3 kwa ajili ya miradi mikubwa ya maji ya Lyamungo-Umbwe, Njiapanda, Tella Mande, Mamba-Mruma, Shimbi Mashariki, Leto na Ngareni. Pia imetoa sh. bilioni 6.3 kwa ajili ya miradi mingine ya visima virefu ya Mweka, Mamba Kusini, Mang'ana, Kyaronga, Kiwaya na Rudugai, Kaloleni, Mkashilingi, Vyanzo vya Kipure, Nikodemo na Mrusungu.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi