loader
Djokovic aomba radhi

Djokovic aomba radhi

NYOTA namba moja wa tenisi duniani, Novak Djokovic, ameomba radhi kwa kumpiga na mpira wa mchezo huo mwamuzi kwenye mchezo wa mashindano ya US Open.

Novak Djokovic alimpiga mwamuzi huyo wakati wa mchezo wa raundi ya nne wa US Open dhidi ya Pablo Carreno Busta na alikuwa amepoteza seti ya ufunguzi kwenye Uwanja wa Arthu Ashe, Marekani.

Raia huyo wa Serbia aligonga mpira nyuma yake kwa kuchanganyikiwa na ukampiga mwamuzi wa kike kwenye koo na kuanguka chini na baada ya tukio hilo Djokovic alikimbia kumwangalia mwamuzi huyo ambaye alikuwa ameumia.

Mwamuzi wa mashindano, Soeren Friemel, alijitokeza na kuzungumza na Mwenyekiti wake, Aurelie Tourte na Andreas Egli ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa mchezo na walifanya mazungumzo marefu na Dkokovic kabla ya kutoa maamuzi.

Mcheza tenisi huyo aliomba msamaha kwa muda mrefu kuwa haikuwa makusudi, lakini baada ya uamuzi kutolewa aliondoka uwanjani.

Djokovic atakumbana na faini nyingine kwa kutofanya mkutano na waandishi wa habari kama utaratibu ulivyo, pia alama zake alizovuna tangu kuanza kwa michuano hiyo zitafutwa ambazo zingeweza kumuweka kwenye viwango vya ubora.

Mpaka anafikia raundi ya nne ya mashindano hayo, Djokovic alikuwa ameshinda michezo 25 mfululizo tangu kuanza kwa mwaka huu. “Kuhusu kutostahiki, ninahitaji kurudi ndani na kushughulikia, kukatishwa tamaa na kugeuza yote haya kuwa somo la ukuaji wangu na mabadiliko kama mchezaji na mwanadamu.”

“Ninaomba radhi kwa mashindano ya US Open na kila mtu aliyehusishwa na tabia yangu. Ninashukuru sana timu yangu na familia kwa kuwa msaada kwangu na mashabiki wangu kwa kuwa pamoja nami kila wakati, asante na samahani sana,” Djokovic aliandika kwenye Instagram.

Kuondoka kwake kwenye mashindano hayo kulimaliza matumaini yake ya kushinda taji la 18 la Grand Slam na kupunguza pengokati yake na Rafael Nadal (19) na Roger Federer (20) katika mbio za kumaliza na ushindi mkubwa kwa wanaume.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ed729b394fe20f7ac8eb4d93a89efdc7.jpg

Klabu ya soka ya Chelsea imefikia muafaka ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi