loader
Uturuki yasikitishwa mahakama kubatilisha hukumu

Uturuki yasikitishwa mahakama kubatilisha hukumu

UTURUKI imesema uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Riyadh, Septemba 7,2020 kubatilisha hukumu ya kifo kuwa kifungo cha miaka 20 jela, uliotolewa kwa waliohusika kumuua mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi huko Istanbul siyo wa haki.

Juzi, mahakama mjini Riyadh iliwahukumu watu wanane kifungo cha miaka saba hadi 20 kwa kuhusika katika mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, aliyeuawa Oktoba, 2018 katika Ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, jijini Istanbul, Uturuki.

Waendesha mashitaka walisema washtakiwa watano wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani, mwingine amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani, wawili wa mwisho wamehukumiwa miaka saba, vyombo vya habari nchini humu vimeripoti.

Desemba mwaka 2018, hukumu tano za kifo zilitolewa katika uamuzi wa awali wa kesi hiyo, na washtakiwa wengine watatu walihukumiwa kifungo cha maisha.

Hata hivyo, juzi Mahakama hiyo ulitoa uamuzi huo wa mwisho na kusema wamebatilisha hukumu ya awali kutokana na familia ya Kashoggi kuwasamehe wahusika wa mauaji hayo.

Saudi Arabia haina mfumo wa sheria uliowekwa na chini ya sheria za Kiislamu, msamaha kutoka kwa familia ya mwathiriwa unaweza kuwa msamaha au adhabu.

Baada ya taarifa nyingi zinazokinzana, mamlaka nchini Saudia imekiri kwamba Jamal Khashoggi, aliyekuwa amekwenda uhamishoni nchini Marekani, aliuawa na viungo vyake vya mwili kukatwa Oktoba 2, 2018 na maofisa wa Saudi Arabia ambao walitenda uhalifu huo bila kutumwa na yeyote.

Mauaji ya Khashoggi yaliyofanywa mwaka 2018 yaliibua hisia na mijadala kila kona ya dunia kutokana na utata wa kifo chenyewe. Awali, Serikali ya Saudi Arabia ilikanusha mauaji hayo kufanywa katika ubalozi mdogo wa Saudia Arabia nchini uliopo Istanbul nchini Uturuki.

Awali kabla ya kutolewa taarifa za mauaji hayo, habari zilisambaa za kutoweka kwa Khashoggi, lakini mchumba wake alitoa taarifa kwamba alimuaga muda mfupi anakwenda Ubalozi wa Saudia Arabia kushughulikia masuala ya ndoa na hakurudi baada ya kuingia ndani.

Picha za video zilianza kusambaa zikimwonesha Khashoggi akiingia katika Ubalozi Mdogo wa Saudia Arabia nchini Uturuki, lakini hakuna picha nyingine wala kamera zilizoonesha akitoka, ndipo utata ukaanza kwamba aliuawa akiwa ndani ya ubalozi huo.

Hata hivyo, baada ya taarifa zake kuanza kusambaa duniani, uchunguzi ulifanywa na hakuna mabaki ya mwili wake yaliyoonekana hadi leo na baadaye nchi hiyo ikakiri kwamba maofisa watano wa nchi hiyo wanahusika na kifo hicho.

Akizungumzia kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Msemaji wa Ikulu ya Uturuki, Fahrettin Altun alisema Saudia imetoa uamuzi wa mwisho kuhusu mauaji ya Kashoggy isivyotarajiwa na ulimwengu na jamii.

Aidha vyombo vya habari viliripoti kwamba mahakama nchini Saudi Arabia iliondoa hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu watano waliopatikana na hatia ya mauaji ya Jamal Khashoggi, mwaka 2018.

Khashoggi alikuwa mwandishi wa habari raia wa Saudi Arabia aliyeishi uhamishoni Marekani na aliuawa kikatili mwaka 2018 baada ya kuingia katika Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia uliopo jijini Istanbul,Uturuki alikokwenda kwa ajili ya kushughulikia masuala ya ndoa.

Wakati sakata la kesi likiendelea, jumuiya mbalimbali za kimataifa zikiwemo wanaharakati wa haki za binadamu walipaza sauti kutaka haki itendeke dhidi ya ukatili huo, huku wengine wakisema serikali ya Saudia inawajibika katika sakata hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5e9674a4c33413fe09640c537ede4186.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: RIYADH, Saudi Arabia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi