loader
Majaribio ya chanjo ya covid-19 yasitishwa

Majaribio ya chanjo ya covid-19 yasitishwa

MAJARIBIO ya chanjo ya covid19 yaliyokuwa yakifanywa na taasisi za afya kwa kushirikiana na kampuni ya dawa iliyotengeneza chanjo hiyo AstraZeneca nchini Uingereza, yamesimamishwa kutokana na madhara yaliyoanza kujitokeza kwa mgonjwa aliyejaribiwa.

Kwa mujibu wa Msemaji wa kampuni ya AstraZeneca, Michele Meixell, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na mgonjwa aliyejitolea kufanyiwa vipimo kuonesha dalili ambazo hazikutarajiwa.

“Tunasitisha kwa hiyari utoaji wa chanjo hiyo ili kuruhusu hatua za uchunguzi kuangaliwa upya na kwa umakini na data za usalama na kamati huru ili tuweze kuja na majibu sahihi ya sababu ya hali hiyo,” alisema Meixell.

Kampuni ya AstraZeneca ambayo ilishirikiana na Chuo Kikuu cha Oxford kutengeneza chanjo hiyo, haikutoa taarifa zaidi kuhusu mgonjwa huyo, lakini baadhi ya vyanzo vya habari vilisema alikuwa ma matatizo mengine katika mwili wake, hivyo yakaleta shida katika kupambana na chanjo hiyo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema karibu chanjo 180 zinafanyiwa majaribio kote duniani, lakini hakuna hata moja iliyofikia viwango vya majaribio ya kimatibabu.

Shirika hilo limesema halitarajii chanjo yoyote itimize miongozo na taratibu za usalama wake na kuidhinishwa mwaka huu, kwa sababu ya muda mrefu unaotakiwa kuifanyia majaribio kwa ajili ya usalama.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a8abbc387088a7ad48be6b3c90314aa0.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, Uingereza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi