loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Manara, Bumbuli kulipa mil 5/- kila mmoja sakata la Morrison

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Nchini (TFF) imempa onyo kali Msemaji wa timu ya Simba, Haji Manara na kumtaka kulipa faini ya Sh milioni tano kwa kukiuka maadili kwa kuisema ovyo Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji juu ya sakata la mchezaji, Bernard Morisson.

Aidha kamati hiyo imemtoza faini ya Sh milioni tano aliyekuwa Mjumbe wa Kamati hiyo Zacharia Hanspope kutokana na kumshutumu Mwenyekiti wa kamati hiyo kwa kutokuwa na maamuzi juu ya kesi ya Morrison.

Naye Ofisa Habari wa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amepigwa faini ya Sh milioni tano kwa kutoa taarifa za uongo kuwa klabu hiyo haijapata nakala za hukumu ya shauri hiyo ilihali klabu ilishachukua nakala.

TIMU ya KMC iliendeleza ...

foto
Mwandishi: Bosha Nyanje

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi