loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

MAGUFULI- HAKUNA UBWABWA WALA BATA LA BURE

MGOMBEA wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi, John Magufuli amesema hakuna mgombea Urais  wa chama chochote cha siasa ambaye atafanya  maendeleo aliyoyafanya hata robo yake.

Magufuli aliyasema hayo katika uwanja wa Mazaina wilayani Chato mkoani Geita katika mkutano wake wa Kampeni za kuwania ngwe ya pili ya kuongoza dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano mingine, baada ya awali kumalizika.

“Sio kila mgombea Urais anaweza kufanya niliyofanya hata robo, huwezi kusema mtakula  ubwabwa wakati hata kwako haukutoshi huo ubwabwa, huwezi kuzungumza mtakula bata hakuna cha bure hata misaafu yote inazungumza asiyefanya kazi na asile,” JPM  akiwa Chato

Aliongeza kuwa, “ Nimefanya mengi kwa miaka mitano, nawaomba watu wa Chato na Watanzania wote nipeni tena miaka mitano, sioni katika wagombea wote wa Urais ambaye anaweza kutekeleza hata robo ya yale niliyofanya, kama mnataka kujaribu jaribuni mtakuja kuniambia.”

MGOMBEA wa nafasi ya ubunge katika jimbo la ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi