loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EU yaahidi kutoa bil 70/- kukabili athari za corona

UMOJA wa Ulaya (EU) umeaidi kuipatia Serikali ya Tanzania Euro milioni 27 ( sawa na Sh bilioni 70), kusaidia kukabiliana na janga la ugonjwa wa homa ya mapafu (Covid-19) inayosababishwa na virusi vya corona na madhara yake kiuchumi.

Rais wa Baraza la EU, Charles Michel alisema hayo jana wakati akipokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Balozi Jestas Nyamanga ambaye ni mwakilishi wa Tanzania EU.

Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya umoja huo Brussels, Ubelgiji. Viongozi hao walikubaliana EU iendelee kutoa ushirikiano kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), kufadhili tafiti zinazolenga kupata chanjo ya Covid -19 na WHO kuwezeshwa kusimamia ithibati ya chanjo zitakazopatikana na ugawaji wake kwa jinsi zitakavyonufaisha nchi zote kwa gharama nafuu.

Michel alisema sehemu ya fedha hizo, zinalenga kuweka miundombinu ya umeme na maji katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizojengwa na serikali kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na virusi vya corona.

“Mipango ya kukamilisha utoaji wa fedha hizo uko katika hatua za mwisho na Umoja wa Ulaya uko tayari kuongeza wigo wa ushirikiano na Tanzania na nchi nyingine Afrika katika kukabiliana na janga hilo pamoja na madhara yake kiuchumi”alisema Michel.

Nyamanga alihimiza umuhimu EU kuondoa marufuku za safari kwa nchi ambazo maambukizi ya Covid-19 yamedhibitiwa ikiwemo Tanzania ili kuwezesha kukua kwa sekta za utalii na nyingine za uchumi.

Alimweleza Michel kuwa vipaumbele vya Tanzania katika nafasi yake ya sasa ya Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) ni kuhakikisha majadiliano yanayoendelea baina ya nchi hizo na EU kuhusu mkataba mpya wa ubia, yanakamilishwa kwa kuzingatia maslahi ya kila upande.

Nyamanga alieleza wito wa nchi za OACPS kuomba madeni yafanyiwe mapitio ili kusogeza mbele muda wa malipo, kubadilishwa masharti ya kulipa au kufutwa kulingana na hali ya uchumi wa kila nchi ili kuwezesha nchi hizo kukabiliana na madhara ya Covid-19.

Alisema, nia ya nchi za OACPS kutaka EU kusitisha kuanza utekelezaji wa kanuni mpya za kusimamia biashara ya bidhaa zinazoingia katika soko la umoja huo kutoka kwao, zilizopangwa kuanza mwakani ili kuzipa nafasi nchi hizo kujipanga baada ya kuathiriwa na COVID-19.

Balozi huyo kwa niaba ya Tanzania alishukuru EU kuendelea kufanikisha jitihada za maendeleo kwa Watanzania kupitia programu kadhaa, ukiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Nchi za Jumuiya ya Ulaya (EDF11).

Tanzania inakamilisha taratibu za kunufaika na awamu nyingine ya mfuko huo wenye takribani ya zaidi ya Sh. bilioni 300 zinazolenga kuimarisha sekta za nishati, kilimo, biashara na maliasil

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi