loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Damu Salama wasaka chupa 32,700 kunusuru wagonjwa

MPANGO wa Damu Salama nchini unatarajia kukusanya chupa za damu 32,700, lengo likiwa ni kuokoa maisha ya wanaopoteza uhai kutokana na kukosa damu, ikiwa ni kampeni maalumu inayoanzia Septemba 21 hadi 25 mwaka huu.

Aidha, katika kipindi hicho kila kanda itakusanya chupa 500 za damu, kila halmashauri chupa 150 na kila mkoa kukusanya chupa 150 za damu.

Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu, Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk Avelina Mgasa alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Damu Salama Uhai wa Mama.”

Alisema kampeni hiyo inahitaji kutoa uelewa kuhusu uchagiaji damu kwa hiari ili kuboresha huduma zinazotolewa katika suala la ukusanyaji wa damu.

Alisema kabla ya mchangiaji kutoa damu, yapo mambo ya msingi ya kuangaliwa ikiwa ni kwa kila mwenye uzito wa kuanzia kilo 50 na kuendelea, lakini pia akipimwa shinikizo la juu na la chini pamoja na kupewa ushauri.

“Katika kampeni hii, Mpango wa Damu Salama utatembelea maeneo ya wazi, shule ili kuhamasisha utoaji wa damu kwa kuwa wapo wagonjwa wanaopoteza uhai kutokana na kukosa damu, hususani wanawake wakati wa kujifungua,” alisema.

Dk Mgasa aliongeza kuwa, hawatapima virusi vya Ukimwi wala homa ya ini, hivyo watu wasiogope kujitokeza.

Alisema uchangiaji damu umekuwa ukiongezeka kuanzia mwaka 2015 ambapo kwa kuhamasisha chupa za damu 196,735 zilikusanywa huku katika mwaka 2020 chupa za damu 39,376 zilikuwa zimekusanywa.

Alisema hilo limefikiwa kutokana na kuimarisha vituo vya damu salama vya kanda na kuzijengea uwezo timu za halmashauri mbalimbali.

Kwa mujibu wa Dk Mgasa, lengo la kampeni hiyo ni hasa kuhakikisha hakuna mjamzito atakayekufa kutokana na kukosa huduma za damu na kwamba, kuanzia mwaka 2015 ukusanyaji damu umekuwa ukifanyika kwa kushirikisha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Aidha, alisema theluthi moja ya wanaofariki ni wale wanaokosa damu na asilimia 18 ya wanawake wanaofariki ni wenye umri wa miaka 18 hadi 45, huku asilimia 50 ya damu yote inayokusanywa ikienda kwa watoto.

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ilemela ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi