loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wajasiriamali Kanda ya  Ziwa waoneshwa fursa

Wajasiriamali Kanda ya Ziwa waoneshwa fursa

WAKUU wa Mikoa ya Mwanza na Geita wamewataka wachimbaji wadogo na wajasiriamali katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutumia ipasavyo maonesho ya dhahabu na teknolojia na taasisi za fedha yanayoendelea mkoani Geita, ili  waweze kujijengea uelewa wa kutosha katika masuala ya fedha na mitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel, walitoa wito huo mwishoni mwa wiki, walipotembelea mabanda ya washiriki wa maonesho hayo, pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye viwanja vya Bombambili.

“Kuna ushiriki mzuri wa taasisi za fedha ikiwamo benki ya NBC ambayo pamoja na kudhamini maonesho haya, pia inaendesha mafunzo kwa wajasiriamali na wachimbaji wadogo.”

“Hii ni hatua kubwa na wito wangu kwa washiriki ni kuhakikisha wanatumia vema fursa hii kujijengea uwezo wa kuendesha shughuli zao kwa ufanisi na kwa viwango bora,’’ alisema Mongella.

Alisema kupitia maonesho hayo, taasisi za kifedha zimetangaza huduma mbalimbali ikiwamo fursa za mikopo kwa ajili ya wadau wa madini wakiwamo wachimbaji wakubwa na wadogo na  wajasiriamali.

Aalisema mafunzo yanayotolewa yatawasaidia wadau hao kujenga uelewa wa kutosha juu ya masuala ya fedha na uendeshaji wa shughuli za madini kisasa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel alisema kupitia maonesho hayo, mkoa huo unatarajia mapinduzi makubwa ya kiuchumi kutokana na mageuzi makubwa ya uendeshaji wa shughuli za kiuchimbaji na biashara yanayotarajiwa kutokana na mafunzo yanayoendelea kutolewa na taasisi mbalimbali kwa wachimbaji wadogo na wajasiriamali.

“Ndio maana tunashukuru sana taasisi za fedha hususani benki ya NBC ambayo ndio wadhamini wakuu wa mafunzo haya. Pia, ushiriki wa taasisi nyingine kwenye mafunzo haya ikiwamo Tantrade, Tume ya Madini, TRA, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, NSSF, GST, Sido, NEMC, TBS, Osha na NEEC, unatuhakikishia mabadiliko tunayoyatarajia kuyapata,” alisema Gabriel.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Serikali katika Benki ya NBC, William Kallaghe, alisema mbali na mafunzo hayo, benki hiyo inaendesha kliniki ya biashara kwa ajili ya wajasiriamali mbalimbali ili waweze kunufaika na mnyororo wa biashara ya madini.

“Ni wingi wa huduma maalumu kwa wadau mbalimbali ndio unaosababisha benki ya NBC tuweze kushiriki kwenye maonesho mbalimbali yakiwamo haya ya dhahabu na teknolojia,” alisema.

Alisema ili huduma za kifedha ziweze kuleta tija kwa wadau wa madini, benki hiyo imeona ipo haja ya kutoa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwasaidia kuzitambulisha fursa za kibiashara ambazo wanaweza kunufaika nazo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/35a26237342e08bbbd8582c3d8604089.JPG

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi