loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kichuya atuliza mashabiki

MCHEZAJI wa Namungo FC, Shiza Kichuya, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na subra katika kipindi hiki ambacho kocha Hitimana Theirry anapambana kutengeneza kikosi chao.

Kichuya ametoa kauli hiyo jana, baada ya kikosi hicho kupoteza mchezo wa pili mfululizo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Rukwa, Kichuya  aliyeingia kipindi cha pili kwenye mechi hiyo kuchukua nafasi ya Abeid Athuman aalisema kikosi cha timu hiyo kinaundwa na wachezaji wengi wageni hivyo siyo kazi rahisi kwa kutengeneza muunganiko katika muda mfupi.

“Mashabiki watakiwa kuwa na subra katika michezo hii ya awali na kumuacha kocha afanye kazi ya kutengeneza kikosi cha ushindani kwani bado tuna michezo mingi pia tuna michezo ya kimataifa,” alisema Kichuya.

Alisema ligi imekuwa na ushindani mkubwa kwani kila mechi, kila timu inapania kuibuka na ushindi hivyo kikosi kikiwa na makosa wapinzani wanatumia fursa hiyo kupata ushindi.

Kichuya alisema bado anaamini kikosi chao kina wachezaji wengi wazuri lakini kocha bado anatafuta kikosi cha kwanza ndio maana hata yeye kwenye baadhi ya michezo amekuwa anaanzia  benchi.

Namungo wamecheza mechi tatu, wameshinda mechi moja kupoteza mechi mbili dhidi ya Polisi Tanzania naTanzania Prisons na kushika nafasi ya 12 kwenye msimamo wakiwa na pointi tatu.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema kupata ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

1 Comments

  • avatar
    Mussa Adamson
    21/09/2020

    Ubelgiji wajipatiaTundulisu Antipasi,ili kujipatia madini ya Watanzania kulipia huduma za Matibabu na kujilimbikizia Mali binafsi,na ni mgombea pekee ambaye ana uraia PACHA,was Tanzania Ubelgiji ndio maana familia yake haipo Tanzania. Na ndio maana anajitapa NCHI HAITATAWALIKA ASIPO SHINDA URAIS.

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi