loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam hii mwendo mdundo

TIMU ya Azam FC imepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Mbeya City kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya jana.

Katika mchezo huo Azam FC walipata bao dakika ya 25 lililofungwa na Ally Niyonzima akiunganisha kona iliyopigwa na Never Tigere.

Huo ni ushindi wa watatu kwa Azam FC, msimu huu na kujukusanyia alama tisa na kukaa kileleni huku Mbeya City wakipoteza mchezo wa tatu mfululizo na sasa inaburuza mkia.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Coastal Union ilitoka suluhu na Dodoma Jiji.

Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi saba sawa na Yanga zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Dodoma Jiji imeshinda michezo miwili na sare moja wakati Coastal Union imepoteza michezo miwili na kutoka sare moja hivyo ina pointi moja katika nafasi ya 16.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema kupata ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi