loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maalim Seif amaliza ziara Pemba

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amekamilisha awamu ya kwanza ya ziara yake ya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kisiwa cha Pemba na sasa anaelekeza nguvu zake Unguja.

Awamu hiyo ya kwanza iliisha mwishoni mwa wiki, ambapo alifanya mikutano mitano ukiwamo wa ufunguzi wa kampeni.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Abeid Khamis Bakar ilisema Maalim Seif licha ya kufanya kampeni za majukwani, alifika katika maeneo ya wananchi na kujionea shughuli zao za kimaisha.

Ilisema mgombea huyo alitembelea maeneo ya kilimo cha mbogamboga, mwani, wavuvi, wafugaji wa kuku  na wafanyabiashara wa maduka mbalimbali.

Katika taarifa hiyo, Abeid alisema Maalim Seif akiwa katika kikundi cha uzalishaji nyanya katika Kijiji cha Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, aliahidi kuwapatia mashine za umwagiliaji maji ili iwe rahisi kuendeleza kilimo hicho na wakulima nao kupata tija.

Alisema hali ya wakulima wengi wa mbogamboga Pemba si nzuri kiafya, kutokana kukosekana kwa vifaa vya umwagiliaji. Alieleza kuwa wakulima wanatumia nguvu kubwa kubeba ndoo za maji vichwani ili kukamilisha kilimo chao.

Kuhusu zao maarufu la mwani, mgombea urais huyo aliwaahidi wakulima hao wanaotumia bahari kufanya kilimo hicho kuwa atahakikisha wanapata boti za kulima mwani mnene, unaolimwa katika maji mengi. Alisema mwani huo unauzwa kwa bei ya Sh 15,000 kwa kilo katika soko la dunia.

“Wazalishaji wengi wa mwani Zanzibar hulima mwani mwembamba kutokana na ukosefu wa vitendea kazi, mwani ambao bei yake haizidi shilingi 1,000,” alisema.

Akiwa Mtambile Wilaya ya Mkoani Pemba, Maalim Seif alielezwa changamoto nyingi zinazowakabili wafugaji, ikiwemo bei za vyakula vya kuku na upatikanaji wa dawa, jambo linalosababisha kuku kufa au kuchelewa kutoa mazao.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Pemba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi