loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cheyo amwombea kura Magufuli

MWENYEKITI wa chama cha  United Democratic Party (UDP), John Cheyo amewaomba wananchi wa Jimbo la Itilima, kumpigia kura mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli kwa kuwa anatekeleza anayoahidi na anajali shida za wanyonge.

Aliyasema hayo katika Kijiji cha Inalo Kata ya Lugulu wilayani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima kupitia UDP, Simon Ngagani.

Cheyo alisema UDP wamekubaliana kumuunga mkono Magufuli kutokana na jitihada zake kusikiliza wanayoyataka wananchi, wakiwamo wanasiasa wa upinzani. Alisema baadhi ya mambo hayo yamo ambayo wanasiasa wa upinzani akiwamo yeye wameyapigia kelele miaka ya nyuma.

"Tuna sababu kubwa ya kumuunga mkono Dk Magufuli kwani kwa kipindi cha miaka yake mitano ya uongozi, tayari ameshatekeleza kwa vitendo sera ya elimu bure, huduma za afya na uboreshaji wa miundombinu rafiki na wezeshi ya biashara,” alisema.

Hata hivyo, Cheyo alisema haridhishwi na mfumo uliopo ununuzi na ulipaji wa fedha za wakulima wa pamba, kwa madai kuwa unachelewesha kupata haki yao.

Mgombea Ubunge Jimbo la Itilima, Ngagani aliwaomba wananchi wamchague ili ashirikiane nao kuliletea maendeleo jimbo hilo.

Ngagani alisema ameacha kazi baada ya kuona changamoto kwenye jimbo hilo, hivyo endapo atachaguliwa atahakikisha anasimamia uanzishwaji wa viwanda na miradi ya maendeleo ili kumaliza tatizo la ajira.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Itilima

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi