loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Kutoichagua CCM ni kupishana na gari la mshahara’

"CCM tumejipanga sawa sawa katika sekta zote hivyo kutokukichagua CCM ni sawa na kupishana na gari la mshahara," amesema mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Miraji Mtaturu.

Mtaturu alikuwa akizungumza na wananchi katika tarafa ya Makiungu na Kata ya Mngaa katika mikutano ya kampeni kuomba wananchi wamchague Rais John Magufuli kuongoza kipindi kingine cha miaka mitano, yeye katika nafasi ya ubunge na madiwani wa CCM.

Alisema Chama Cha Mapinduzi kiko vizuri na kimejipanga kiuongozi katika sekta zote, hivyo kuacha kukichagua ni kupoteza fursa za maendeleo kama kupishana na gari la mshahara.

Aliwaomba wananchi jimboni humo kumchagua ili apate fursa ya kufanya mambo makubwa kwa faida ya jimbo hilo. Alisisitiza kuwa kugombea ubunge si kujaza nafasi, bali ni uwakilishi makini na kuwatumikia wananchi kwa kuwapelekea maendeleo.

Mtaturu alisema anataka kuacha alama ya utendaji, kama alivyofanya katika maeneo mbalimbali alikoaminiwa kufanya kazi. Aliahidi kuwa atahakikisha jimbo hilo linakuwa la mfano kwa  majimbo yote nchini katika suala la maendeleo.

Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 imebeba matumaini na ina majibu ya kero zinazowakabili Watanzania.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,  Juma Kilimba alisema uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu, hivyo wananchi wamchague rais ambaye atawafaa Watanzania.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa alisema wagombea kutoka CCM wanastahili kuchaguliwa kwa kuwa chama hicho kina sera na dira kwa faida ya taifa.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Singida

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi