loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wagombea pigieni chepuo usalama barabarani

KWA sasa nchi nzima zinaendelea kampeni za vyama vya siasa kuaomba kuchakuguliwa kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Vyama mbalimbali vimesimamisha wagombea kuwania nafasi za uraisi, udiwani na ubunge kupitia uchaguzi huo.

Wagombeawamekuwa wakifanya kampeni kila kukicha kuanzia Agosti 26, siku ambayo zilianza rasmi na zitamalizika Oktoba 27 saa 12 jioni, hivyo ni kampeni ya miezi miwili.

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kampeni hizo kuanzia kusikilia kwenye radio, kuangalia kwenye luninga, kusoma kwenye magazeti, kufuatilia katika mitandao ya kijamii na hata wakati mwingine kuhudhuria mikutano hiyo, lakini ninasikitika sijasikia wagombea wakigusia namna ambavyo wataimarisha suala zima la usalama barabarani.

Imekuwa ni kawaida kusikia wagombea wakigusia watakavyoimarisha elimu, afya, kupanua wigo wa ajira ili kuwaendeleza vijana, uanzishwaji wa viwanda na mengineo kadhaa ambayo kimsingi nayo ni ya muhimu.

Lakini, napenda kuwashauri wagombea kupigia chepuo namna watakavyoimarisha suala la usalama barabarani, kwa maana nyingine watakavyozuia madhara yatokanayo na kukosekana kwa mazingira bora ya usalama barabarani.

Kukosekana kwa mazingira hayo kunasababisha ajali za barabarani na kupelekea idadi kubwa ya vifo, pamoja na majeruhi wengi.

Wagombea wanapaswa kutambua kuwa, wanaokufa na kujeruhiwa ni kati ya wapiga kura wao, hivyo basi kama ajali zikiendelea idadi ya wapiga kura inapungua.

Hata hivyo, ninatambua upo muingiliano wa sera za wagombea na hoja ya usalama barabarani, ingawaje sio wa moja kwa moja. Mfano, kama mgombea akijinadi kuwa ataimarisha miundombinu ya barabara ni wazi hata usalama barabarani utakuwa umeimarika kwa kuwa kama barabara zikiwa bora kwa maana zikawa na alama za barabarani, zimejengwa kwa ufanisi usalama unaweza kuwa mkubwa zaidi.

Hivyo nitafarijika zaidi kama nikisikia wagombea hao wakigusia masuala mengine mbadala kuhusiana na usalama barabarani, mfano mgombea akijinadi namna atakavyochagiza maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani ya 1973 ambayo imepitwa na wakati.

Hapo hakika mgombea atakuwa ameonesha nia ya dhati ya kusaidia uimarishwaji wa usalama barabarani, kwani sheria ikitungwa mpya inayoendana na wakati itachagiza kuimarisha usalama barabarani kwa kuwa itatoa mwongozo wa nini kifanyike, huku ikiainisha adhabu kwa watakaokiuka mwongozo.

Hakika matumizi ya barabara yasipokuwa salama kwa maana ya kukiwa na madereva wanaoendesha kwa mwendo kasi zaidi ya kiwango kinachotakiwa, wakiendesha huku wakiwa wamelewa au wakiendesha bila ya kuzingatia masharti mengine, ni wazi matumizi bora ya barabara yanabadilika na kuwa matumizi hatari.

Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo zinatekeleza mradi wa Bloomberg unaofadhiliwa na Shirika la Afya Duniani, ambao unaangazia matumizi bora ya kofia ngumu (helmet), matumizi ya viti vya watoto, uvaaji wa mikanda, kiwango cha unywaji wa pombe kwa madereva na mwendo kasi.

Kuna haja ya wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kuhamasisha matumizi bora ya barabara kwa maana ya matumizi bora ya helmet, mikanda na mengineyo kama yanavyoelekezwa kwenye mradi huo ili kuinusuru jamii dhidi ya athari zinazotokana na kukosekana kwa matumizi sahihi ya usalama barabarani.

KATIKA kipindi cha miezi michache iliypopita, dunia ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi