loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahakama ya Jiji kuanzishwa Dodoma

JIJI la Dodoma liko katika mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Jiji, ili wote watakaokiuka taratibu mbalimbali za mazingira, wachukuliwe hatua na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Mdhibiti wa takangumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dikson Kimaro.

Alisema hayo wakati wa  zoezi la kufanya usafi kwenye maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani, inayofanyika Septemba 19 ya kila mwaka.

Kimaro alisema Jiji la Dodoma lipo katika mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Jiji, hivyo wote watakaokiuka kanuni za kimazingira, hatua zitachukuliwa kwa kufikishwa katika vyombo husika kwa mujibu wa sheria.

Aliwataka wakazi wa jiji hilo, kujiepusha na tabia ya kutupa taka hovyo katika maeneo ambayo siyo rasmi. Alisema atakayebainika kufanya hivyo, sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.

Alisema Jiji la Dodoma likinatakiwa kuwa la mfano, kwa kuzingatia usafi wa mazingira na watu wanatakiwa kuacha kutupa taka ovyo.

Alisema Jiji hilo limeweka mikakati mbalimbali, kuhakikisha linakuwa safi na watu wanazingatia kanuni za usafi.

 Alisema ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanakuwa walinzi namba moja wa kulinda mazingira, kwani Jiji peke yake haliwezi kuwa mlinzi bila kuwa na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi.

Alisema hata wasafiri wanatakiwa kuacha kutupa taka ovyo wanapokuwa kwenye vyombo vya moto. Wananchi wanatakiwa kuwafanya usafi kwenye nyumba wanazoishi. Alisema Jiji litaendelea na utaratibu wake wa kuhakikisha usafi unafanyika kila siku ya Jumamosi.

Alisema kwa mujibu wa sheria ndogo  ya Jiji mtu akikamatwa anatupa taka ovyo faini ni kuanzia Sh 50,000 hadi Sh 300,000.

Meneja wa Tawi la Green Waste Jiji la Dodoma, Abdallah Mbena alisema maeneo ambayo wamekuwa wakiyafanyia usafi huwa yana wafanyabiashara  wengi na mara nyingi yamekuwa yakichafuliwa na watu.

 

Malick Masudi Mkazi wa Bahi Road, alisema usafi ni muhimu kufanyika hivyo usiishie hapo tu bali uwe mwendelezo, kwani suala la usafi si la watu fulani, bali kila mtu ana wajibu na jukumu la kuweza mazingira katika hali ya usafi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Viwandani nao walishiriki  kufanya usafi katika maadhimisho hayo, wamesema usafi wa mazingira ni muhimu kufanyika kwani husaidia kujiepusha na magonjwa ya mripuko ambayo hutokana na uchafu.

Usafi huo ulianzia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma hadi Soko Kuu la Majengo.

Maadhimisho ya siku ya Usafi Duniani yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Plastiki yako, Mazingira yetu’.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi