loader
Majaliwa: ACT, Chadema mchagueni Dk Magufuli

Majaliwa: ACT, Chadema mchagueni Dk Magufuli

"Tunataka kiongozi atakayelinda rasilimali za taifa hili. Na huyo si mwingine bali ni Dk John Magufuli. Tunataka kiongozi atakayeweza kuongoza nchi. Wewe mwanachama wa ACT, CHADEMA, NCCR au CHAUMA, mchague Dk John Magufuli awe Rais kwa sababu maendeleo hayachagui chama," amesema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Kata za Issenye na Natta waliojitokeza kumlaki wakati akienda Mugumu, Serengeti mkoani Mara kufanya kampeni kuwaombea kura wagombea wa CCM.

"Hiki siyo kipindi cha kujutia maamuzi au cha kufanya majaribio ya uongozi. Chagueni kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza nchi. Usimchague mtu tu hata kama ni mtoto wa dada yako" alisema Majaliwa ambaye pia anawania nafasi ya Ubunge kwenye jimbo la Ruangwa. 

Katika mkutano huo, aliwaombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Serengeti, Amsabi Mhimi na wagombea udiwani wa Kata za Issenye na Natta, Mosi Nyarobi na Juma Porini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9fe2d367afa9de64e71c61232f1ffc73.jpeg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi