loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijana wahimizwa kuchukua mikopo

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza, Dk Angelina Mabula (pichani) amewashauri vijana kupitia vikundi vya ujasiriamali.

Rai hiyo ilitolewa na Dk Mabula katika mkutano wake wa kampeni katika viwanja vya Mecco Kaskazini. Dk Mabula alisema halmashauri hiyo ilitenga Sh bilioni 1.3 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Dk Mabula alisema ni vikundi 24 vya akinamama vimepewa mikopo katika Kata ya Mecco. Aliwapongeza wakazi wa Ilemela kwa kuchangia Sh milioni 311 kwa ajili ya kuchangia sekta ya elimu katika kipindi cha mwaka 2015-2020.

Alisema fedha zilizochangwa na wananchi katika sekta ya elimu, zimetumiwa ipasavyo.

Alisema Kata ya Mecco imejitahidi kurasimisha ardhi, ambapo katika mtaa wa Nundu wakazi 902 walipewa hati. Alisema hati 31,936 zimetolewa kwa wilaya nzima.

Alisema katika Kata ya Mecco Sh milioni 397 zimetumika kulipa fidia ya ardhi kwa wakazi, ambao maeneo yao yalichukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za kata.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi