loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yapewa mbinu kunusuru uchumi

WATAALAMU wa uchumi nchini wameishauri serikali kutumia wataalamu kunusuru uchumi wa nchi unaotishia kuanguka.

Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Sudan Kusini zinaonesha kuwa, kushuka kwa pauni ya nchi hiyo kumesababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu sokoni, huku Aprili mfumuko wa bei ukifikia asilimia 3.2 kutokana na uchumi kutegemea mapato ya mafuta yaliyoshuka bei kwa kiasi kikubwa duniani.

“Tunaona kuwa serikali haijafanya kazi yake ipasavyo katika sera za kiuchumi, hakuna sera nzuri za uchumi kwa kuwa wachumi wamepuuzwa katika mchakato wa kutoa maamuzi,” amesema.

Wataalamu hao wa uchumi wameilalamikia serikali kwa matatizo ya uchumi kuwa imekuwa ikidharau mapendekezo yanayotolewa na wataalamu wa uchumi katika kukabiliana na mgogoro wa uchumi uliopo.

“Kuongezeka kwa thamani ya dola ya Marekani ni janga, kwani imesababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa katika masoko, hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka,” alisema Ajieth, mmoja wa wataalamu wa uchumi nchini humo.

Alisema bei ya nyama ya ng’ombe kwa sasa ni pauni 1,200 kwa kilo, wakati awali ilikuwa ikiuzwa kwa pauni 1,000, huku bei ya nyama ya mbuzi ikiwa pauni 2,000 kwa kilo, wakati kilo ya mahindi imeongezeka bei mpaka pauni 600 kutoka pauni 300.

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi