loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mgombea CUF aahidi stendi, lami Maramba

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mkinga kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Nuru Bafadhili amesema endapo atachaguliwa, atahakikisha Tarafa ya Maramba inapata stendi na atapeleka umeme kwenye vijiji visivyokuwa na nishati hiyo.

Ametoa ahadi hiyo jana kwa wananchi wa vijiji vya Migombani, Milenane, Mwakijembe na Matemboni pamoja na Maramba mjini kwenye mikutano ya kampeni.

Alisema kwa muda mrefu tarafa hiyo imekuwa haina kituo cha mabasi, hivyo kusababisha ajali za mara kwa mara katika eneo hilo. Alisema akiwa mbunge atashirikiana na Halmashauri ya Mkinga ili kupata eneo maalumu la kujenga stendi ya kisasa.

“Nikiingia madarakani jambo nitakaloanza nalo ni ujenzi wa stendi ambayo ndio kero kubwa katika eneo hili, lakini pia ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Tanga mjini hadi hapa Maramba, kwani wakati wa mvua barabara hii haipitiki” alisema Bafadhili Mgombea huyo pia alisema atahakikisha ujenzi wa soko unaanza haraka iwezekanavyo.

Alisema yupo tayari kuchangia gharama za ujenzi huo ili kusaidia kuongeza ajira kwa wananchi.

Bafadhili pia aliahidi ujenzi wa machinjio katika eneo la Maramba, kwa kuwa wananchi wanalazimika kufuata huduma hiyo makao makuu ya wilaya, ambako ni mbali.

“Wamejenga machinjio makao makuu ya wilaya, ambako hakuna idadi kubwa ya wanyama wanaochinjwa, wakati hapa kwa siku moja mnachinja mbuzi 15.

Huko waliko na machinjio hata mbuzi 10 hawafiki kwa siku moja “ alisema. Awali vijiji vya Migombani na Milenane Kata ya Mwakijembe, mgombea huyo alisema atahakikisha vijiji hivyo vinapatiwa umeme, maji na zahanati ili wananchi wasisafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizo.

Alisema anatafuta wahisani ambao kwa kushirikiana na halmashauri, wachimbe visima ili kupunguza ukosefu wa majI

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Amina Omari, Mkinga

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi