loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kauli ya Ndayishimiye itamaliza ukabila EAC

UKABILA ni tatizo linalozitafuna baadhi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na limesababisha mitafaruku, kupigana vita na wananchi kukimbia nchi zao na kujihifadhi katika nchi jirani.

Baadhi ya nchi za EAC ambazo zinasumbuliwa kwa muda mrefu na tatizo sugu la ukabila tangu kupata uhuru wao ni Burundi, Kenya, Sudan Kusini na Rwanda.

Juhudi za makusudi za hivi karibuni zinazochukuliwa na viongozi wa mataifa hayo kupambana na kirusi cha ukabila, zinaleta matumaini ya kumaliza tatizo hilo katika Afrika Mashariki.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini, alisema kwa sasa Warundi ni wamoja, hakuna cha Mhutu wala Mtutsi, wote wanashirikiana kujenga nchi yao.

“Tumegundua kwetu Burundi hatuna kabila la Kihutu na Kitutsi, tukagundua kuwa ni wazungu walitugawa tu bila sababu ya msingi kwa sababu kabila hapa ni Warundi wanaozungumza Kirundi na nchi yetu ni Burundi, hatutarudi tena katika machafuko ya zamani,” alisema Rais Ndayishimiye.

Hii ni kauli ya kishujaa yenye matumaini makubwa ndani yake, ambayo ikitekelezwa kama Rais Ndayishimiye alivyoahidi, ni dhahiri amani ya kweli itapatikana Burundi baada ya miaka mingi ya vita na machafuko.

Msimamo wa Ndayishimiye wa kuwaongoza Warundi katika umoja wa kitaifa, ni mfano mzuri kwa nchi yake na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Hali hiyo itasaidia kumaliza uhasama nchini humo na kuleta amani ya kudumu. Si Burundi peke yake iliyoanzisha harakati za kujenga umoja na uzalendo.

Kenya nayo imeanza juhudi za kuangamiza ukabila. Juhudi hizo zinaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na zinachukuliwa baada ya nchi hiyo kwa muda mrefu kuteswa na ukabila hadi kusababisha machafuko, hasa baada ya uchaguzi mwaka 2007.

Rais Kenyatta kwa kuonesha mfano, yeye kutoka kabila la Kikuyu alimaliza tofauti yake na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga, kutoka kabila la Wajaluo.

Kupitia Mpango wa Kuunganisha Taifa maarufu BBI, Rais Kenyatta analenga kuondoa ukabila, udini, ukanda na matabaka mbalimbali kati ya jamii za nchi hiyo.

Hii ni fursa nzuri kwa taifa la Kenya kufikia muafaka wa kitaifa. Sisi wana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tunaiona hali hiyo kama ni kitendo cha kuzika kabisa tofauti za kikabila na machafuko yoyote, yanayosababishwa na chaguzi mbalimbali katika taifa hilo na nchi jirani

ZIMEBAKI siku nne kufi kia siku ya Uchaguzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro, Tudarco

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi