loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sven ataka mkataba mpya kwa Chama

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema kwa maoni yakeatafurahia kama Clatous Chama ataongezewa mkataba ili aendelee kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu.

Sven alisema hayo baada ya Chama kuonesha kiwango kikubwa na kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa juzi. 

Alisema anajua mkataba wa mchezaji huyo unamalizika Julai, mwakani na kama kiwango chake kitaendelea kama anavyofanya sasa atafurahi akiongezewa mkataba. 

“Mawazo yangu ningefurahi kumbakisha kwa kiwango anachoendelea kukionesha kwa sasa, kama kocha ninafuraha kuwa naye sehemu ya kikosi, ana ubunifu na anafanya kazi inayotakiwa, sio kwa mimi ni kwa kocha yeyote hawezi kuona mchezaji mzuri anaachwa.” 

 “Kikubwa mimi kama kocha sina maamuzi makubwa, ila yapo mikononi mwa timu na mchezaji mwenyewe, siwezi kujua anachowaza Chama au Bodi ya Simba, wanachofikiria kwa sasa juu ya kumuongeza mkataba Chama,” alisema Sven.

Aidha, kocha huyo alisema anafurahishwa na kiwango kinachoendelea kuoneshwa na  kiungo Mzamiru Yassin.

“Nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu kwenye mechi ya leo (juzi), Mzamiru Yassin kanifurahisha sana, mechi zilizopita alifunga mabao mawili na ametoa pasi za mabao kwenye mechi ya leo (juzi), sasa inanipa nguvu ya kujiamini kwa kila mchezaji kwenye kikosi changu kuwa anaweza kufunga,” alisema Sven.

Alisema kikubwa anafurahi kupata ushindi mnono na baada ya kuruhusu kufungwa mabao mechi zilizopita, kwa sasa hawezi kumtegemea mchezaji mmoja kufunga.

 “Sasa nina vyanzo tofauti vya kupata mabao na hii inanifanya kuwa makini kuangalia wachezaji wanaofanya vizuri zaidi kwenye mazoezi, nataka kutengeneza kikosi bora kulingana na mazingira ya uwanja tunaoenda kutumia,” alisema.

Kwenye mchezo huo, Chama alifunga mabao mawili na mengine yakifungwa na Meddie Kagere na mshambuliaji mpya aliyeanzia benchi, Chris Mugalu.

Kwa upande wake, Kocha wa Biashara United, Francis Baraza, alisema amekubali matokeo hayo na kuahidi kujipanga upya ili kufanya vema kwa kufuta makosa yaliyowafanya kupoteza mechi hiyo.

“Kwenye mechi ya leo (juzi) tulizidiwa kimbinu, wapinzani wetu walikuwa bora kwenye kila idara, kikubwa tunaenda kujipanga upya kuangalia mechi zinazokuja kuona tunapata matokeo mazuri,” alisema. Baraza alisema wakati wanaingia kwenye mechi hiyo, malengo yao yalikuwa ni kutafuta sare, lakini wapinzani wao waliwafanya washindwe kufanya lolote.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema kupata ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi