loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TARI yaombwa kufanya mafunzo mara kwa mara kwa wakulima

WAKULIMA wa korosho wilayani Masasi wamekiomba Kituo cha utaftii wa kilimo nchini  (TARI) kuendele kutoa mafunzo ya kuimarisha kilimo cha korosho kwa wakulima hao mara tatu kwa mwaka ili wakulima waweze kujua na kufuatilia ulimaji na mbinu bora za kilimo cha zao la korosho.

“Tunashauri semina ya namna hii iwe inafanyika kwa mwaka mara tatu, kipindi cha maandalizi ya shamba, kipindi cha upulizaji wa dawa na kipindi cha kuokota korosho,” amesema Maida Rashid, mkulima wa korosho Masasi.

Amesema kilimo cha korosho kinabadilika kila mara kutokana na sababu mbalibali zikiwemo sababu za mabadiliko ya hali ya hewa ambapo hali hiyo husababisha kuibuka kwa magonjwa na wadudu mbalimbali ambao hushambulia zao hilo.

“Tunaomba watafiti hawa wa TARI kutoa mafunzo kwetu sisi mara tatu kwa mwaka ili sisi wakulima tuweze kuendelea kupata mbinu za kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa,” amesema Amina Salum.

Akizungumza wakati anatoa mafunzo ya kilimo bora cha zao la korosho kwa wakulima hao, Mtafiti upande wa wadudu na magonjwa kwa mikorosho Dadili Majune, aliwaomba mabwana shamba wakiwemo maafisa ugani kuwatembelea wakulima wa korosho  shambani mara kwa mara ili kuwapa elimu sahihi kuhusu ulimaji na ukuzaji bora wa korosho.

Majune amesema mabwana shamba wengi huwa hawatembelei wakulima na kuwapa elimu sahihi kuhusu viwatilifu sahihi na njia sahihi ya kukabiliana ugonjwa na wadudu wanaoshambulia mikorosho.

“Mabwana shamba ndiyo wenye jukumu la kuwatembelea na kuwapa wakulima elimu sahihi na matumizi sahihi ya viwatilifu, lakin wengi wao hawafanyi hivyo,” amesema.

Majune ameongeza kuwa hatua hiyo imekuwa ikiwalazimu wakulima wengi kununua viwatilifu na kutumia visivyo katika kuundoa wadudu na kutibu magonjwa ya mikorosho.

Amesema mabwana shamba na bibi shamba wanatakiwa kuwepo mashambani kila mara na kuwasaidia wakulim njia bora za kuboreshe zao la kilimo.

Kwa upande mwingine Dadili ameiomba serikali kuoogeza maafisa kilimo nchini ili waweze kuwa wengi kusaidia wakulima katika kukuza kilimo. Amesema maafisa kilimo waliopo hawatoshi kusaidia wakulima wote nchini.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Anne Robi, Lindi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi