loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk. Mabula aahidi umeme Kahama

MGOMBEA wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Ilemela, Dk Angelina Mabula amewaahidi wakazi wa kata ya Kahama kuwa upatikanaji wa umeme halitakuwa tatizo tena katika kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Lukobe. Dk Mabula alisema Serikali imetenga bilioni 12 kwajili ya kuweka umeme wilayani Ilemela. 

Alisema wakazi wa Kata hiyo watawekewa umeme katika mitaa yote. Aliahidi umeme utawekwa pia katika zahanati ya Lukobe.  Alisema Jimbo la Ilemela lina mitaa 171 ni mitaa 56 tu ndio haina umeme.

Alifafanua kuwa katika sekta ya Ardhi, mtaa wa Lukobe na Buduku jumla ya shilingi bilioni 6.2,  zimelipwa kama fidia kwa wananchi.

 Dk. Mabula aliongeza kuwa wakazi 1892 katika mtaa wa Kahama wamechukua hati zao, mtaa wa magaka waliochukua hati ni 567 na mtaa wa Isela waliochukuwa ni 11. Alisema milioni 68 zimetolewa kama mkopo kwa vijana, wanawake walemavu.

Alizungumzia kuhusu miundombinu ya barabara kuwa wametenga bilioni 180 kwajili ya ujenzi wa Barabara ya Kahama- Isela, Bulale-Ilalila na Igogo-Sangabuye.

Katika sekta ya elimu Dk. Mabula alisema katika kipindi cha miaka mitano Serikali wilayani Ilemela imefanikisha ujenzi
wa maabara13, madawati 7605 kwa shule za msingi na madawati 3640 shule za sekondari.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi