loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KMC yaishusha Azam kieleni

TIMU ya KMC iliendeleza wimbi la ushindi kwa mchezo wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mwadui FC mabao 2-1, mechi iliyofanyika Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga jana.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani muda wote, KMC iling’arishwa kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Reliant Lusajo katika dakika ya 77 na 84, wakati Mwadui walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 11 kupitia kwa Issa Shaban.

Ushindi huo umewafanya KMC kukalia usukani wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18 msimu huu, baada ya kufikisha pointi tisa kutoka katika mechi tatu walizocheza hadi sasa na kuishusha Azam FC iliyokuwa ikiongoza kwa tofauti ya wingi wa mabao ya kufunga.

KMC inaendelea kuweka rekodi yake, kwani tangu ligi imeanza kila raundi inavyo kamilika imekuwa ikikalia usukani wa ligi hiyo, ambapo sasa wamebebwa na wingi wa mabao baada ya kufunga mabao nane na kufungwa mawili.

Katika mchezo mwingine wa kukamilisha raundi ya tatu uliopigwa jana, Ruvu Shooting ilichomoza na pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Gwambina FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Katika ushindi huo wa kwanza kwa Ruvu Shooting baada ya kupoteza mechi moja na kusuluhu nyingine, walipata bao hilo pekee kupitia kwa Fully Maganga katika dakika ya 40.

Matokeo hayo yanawafanya Ruvu Shooting kufikisha pointi nne, wakishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wakishinda mechi moja, sare moja na kupoteza mmoja, wakati wapinzani wao Gwambina, wenyewe wameendelea kuyumba baada ya kufungwa mara mbili na kutoka suluhu mara moja, hivyo kujikusanyia pointi moja kutoka katika mechi tatu.

Gwambina wametoka suluhu dhidi ya Kagera Sugar, wakafungwa dhidi ya Ruvu Shooting na Biashara United.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema kupata ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi