loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Biteko ataka Brela kudhibiti vishoka mtandaoni

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko ameutaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutumia weledi kutatua changamoto ya vishoka wa mitandaoni wanaowasumbua wafanyabiashara wanaotaka kusajili majina na alama za biashara.

Alisema hayo jana alipotembelea banda la Brela katika Maonesho ya Dhahabu na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

“Nawapongeza Brela kwa kutatua tatizo la kampuni hewa na migogoro ya kampuni, changamoto kubwa ambayo bado ipo ni vishoka wanaosumbua katika mitandao, naomba mwendelee kulishughulikia hilo,” alisema.

Aidha, aliipongeza Brela kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini na kuongeza kuwa, imekuwa ikitoa ushirikiano wa haraka mara wanapohitajika kufanya hivyo.

Alitolea mfano wa ushirikiano uliofanywa na Brela kwa Wizara ya Madini uliofanikisha kutatua tatizo la kampuni hewa na migogoro hususani kampuni ya uchimbaji madini ya Nyarugusu.

Kwa mujibu wa Waziri Biteko, ushirikiano uliotolewa na Brela kwa Wizara ya Madini, uliwezesha kwa kiasi kikubwa kutatua mgogoro huo.

Katika pongezi zake, alisema Brela inafanya kazi nzuri kuhakikisha matatizo yanatatuliwa kwa wakati hasa baada ya kuweka mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao uliopunguza changamoto nyingi kwa wafanyabiashara na kuwawezesha kupata hudumu haraka na kwa wakati.

Waziri Biteko alisema matarajio ya serikali ni kuona wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo wanaachana na uchimbaji wa kutumia majina yao, badala yake wanasajili kampuni zitakazowaongezea tija na kuwawezesha kulipa kodi na kuchangia katika pato la taifa.

MCHICHA ni aina nyingine za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi