loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa ajivunia punguzo kodi sekta ya uvuvi

Majaliwa ajivunia punguzo kodi sekta ya uvuvi

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015 -2020 ilielekeza kupunguza kodi kwenye sekta ya uvuvi, na agizo hilo limetekelezwa.

 Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Bukima, wilayani Musoma, Mara katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Majita.

 Katika mkutano huo, Majaliwa alimuombea kura mgombea urais kupitia CCM, John Magufuli, mgombea ubunge jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo na wagombea udiwani kupitia chama hicho.

"Katika kutekeleza Ilani ya CCM, tumepunguza kodi kwenye malighafi na zana za uvuvi, kwenye injini za uvuvi, nyuzi za kushonea nyavu za kuvulia samaki, vifungashio na kwenye ada za leseni za kuvulia samaki,"alisema Majaliwa.

Alisema mambo mengine yaliyofanyika kwenye sekta ya uvuvi kuwa ni kuwatambua wavuvi na kuwaweka kwenye vikundi hivyo kuviongeza kutoka 37 hadi 113.

 "Ni kwa nini tuliamua kuwaweka kwenye vikundi, ni kwa sababu inakuwa rahisi kuwafikia, kuwaelimisha na kuwahudumia. Hii imefanikisha idadi ya samaki wanaovuliwa iongozeke kutoka samaki 415,000 hadi kufikia zaidi ya 800,000," alisema  Majaliwa.

Kwa mujibu wa Majaliwa kiwango cha uvuaji samaki kimeongezeka kutoka tani 300 na kufikia tani 448, 467. "Kikubwa ninachowaomba ni kwamba, tumieni vyombo vya kisasa kuvua samaki ili kutunza mazalio yao".

 Akiwa njiani kuelekea Musoma Mjini, Majaliwa alisimamishwa na wakazi wa kata za Kusenyi, pia aliwasalimia wakazi wa kata za Mugango na Mkirira, ambako pia aliwaombea kura wagombea wa urais, ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Musoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi