loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mikoa 23 Tanzania Bara rasmi kuanza mabucha nyamapori

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imetangaza kuanza kwa bucha za kuuza nyamapori katika  mikoa  23 ya Tanzania bara.

Kutangazwa rasmi kuwepo kwa bucha hizo ni baada ya kupata maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Rais John Magufuli  mnamo Januari 3 mwaka huu (2020) wakati akiwa ziara ya kikazi Mkoani Rukwa.

 Katibu mkuu wa Wizara  ya Maliasili na Utalii ,Dk Aloyce Nzuki alitangaza hatua ya kuanzishwa kwa bucha hizo  jana ( Sept 25)  akiwa katika Ofisi za makao makuu ya  TAWA yaliyopo mkoani Morogoro.

Dk  Nzuki , alisema  kuanzishwa bucha za kuuza nyamapori ni fursa kwa wananchi  na  ni matakwa ya Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2007 na sheria ya kuhifadhi wanyamapori sura namba 283.

"Sheria hii imehimiza wananchi kutumia na kunufaika moja kwa moja au shughuli za utalii zinazoiletea Serikali mapato kupitia matumizi kwa endelevu ya rasilimali ya wanyamapori,"alisema Dk Nzuki.

Watanzania 4,247 wamepata ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi