loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samatta bado ana nafasi ya kung’ara Uturuki

GUMZO kubwa kwa wanasoka wengi  nchini ni mshambuliaji  wa klabu ya Aston Villa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta  kuwasili katika mji wa Istanbul ili kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwa klabu ya Fenerbahce. 

Nyota huyo raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 27  alijiunga na Villa akitokea Genk Januari mwaka huu na kufunga jumla ya magoli mawili pekee kwenye michezo 16 aliyocheza chini ya kocha Dean Smith.

Mara kadhaa klabu ya Fenerbahce imekuwa ikihusishwa kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo hatari wa Taifa Stars tangu walipoona hatma yake ndani ya Villa si nzuri kwa kuanzia benchi kwenye baadhi ya mechi muhimu.

Hata hivyo, West Bromwich Albion walikuwa pia kwenye rada  wakihusishwa na mchezaji huyo, ambaye kwa sasa inadaiwa tayari ameshatua katika jiji la Istanbul kukamilisha dili hilo la mkopo wa mwaka mmoja na Fenerbahce, huku wakiwa wanayo nafasi ya kumnunua moja kwa moja.

Ndoto ya Samatta na watanzania kwa muda mrefu walikuwa kwenda kucheza soka kwenye Ligi Kuu ya England kwa kuwa Watanzania wengi wanafuatilia licha ya mambo kwenda kama yalivyopanga lakini maisha aliyaanza vibaya.

Villa ambayo msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja ilimsajili Samatta kwa lengo la kwenda kutimiza wajibu wake kwenye kufunga, lakini kwa michezo aliyocheza hususani ile muhimu alishindwa kuonesha makali yake kwa sababu mbalimbali.

Kwanza alikuwa anatakiwa apewe muda wa kujenga maelewano na wachezaji aliowakuta, lakini nafasi hiyo haikuwepo kwa kuwa Villa ilikuwa kwenye presha kubwa ya kutafuta matokeo mazuri kujinusuru.

Pamoja na changamoto hiyo, Villa walifanikiwa kuvuka salama wakati wanajiandaa kwa msimu mpya wamesajili wachezaji wengi ambao wanacheza kwenye namba ya Samatta na Samatta kutolewa kwa mkopo kwenda kutafuta changamoto mpya.

Kutolewa kwa Samatta kwenda kwa mkopo si mwisho wa  kuendelea kucheza soka, kwani anaenda kwenye timu ambayo itamfanya kuonekana kwenye michuano mikubwa  ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya, anaweza kuonesha makali na akarudi tena England.

Ni wazo kutolewa kwake kwa mkopo kuwe chachu kwa wanasoka wetu  ya kuendelea kuamini kwamba hata wao  wana uwezo wa kwenda kucheza soka la kulipwa kama watacheza kwa kutambua mpira ni ajira yao rasmi.

Samatta amefungua njia kwa watanzania, sasa ni wakati wa wachezaji chipukizi  kupambana wakiwa na umri mdogo kusimamia malengo yao kwa kufika mbali kuzidi mafanikio aliyoyafikia Samatta.

ZIMEBAKI siku nne kufi kia siku ya Uchaguzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi