loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbao FC, yajipanga upya Ligi Daraja la Kwanza

 KOCHA mkuu wa timu ya ligi daraja la kwanza(FDL) Mbao FC,Almas Mosha’Kiongozi’ amesema kwa sasa timu yake inaendelea vyema na maandalizi ya michezo yake ya ligi daraja inayptarajia kuanza mwezi ujao.

Akizungumza na mtandao huu, Almas alisema timu yake inaendelea vyema na mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba wilayani Ilemela.

Kocha huyo wa zamani wa Gold Sports FC na Toto Africans alisema ana imani kubwa sana na kikosi chake kitafanya vyema katika ligi daraja la kwanza(FDL) kutokana na uwezo wa  wachezaji alionao.

Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza waendelee kuungana kwa pamoja katika kuisaidia timu yao ili iweze kurejea tena katika ligi kuu. Aliahidi atahakikisha timu yao inacheza mechi ya kirafiki ili kuweza kujipima ubavu.

Baadhi ya wachezaji 25 waliosajiliwa na Mbao FC katika ligi daraja la kwanza msimu huu ni Rajesh Kotecha, Hamis Kasanga,Ndaki Robert,Bruno John,Henry Shindika,Ayoub Mwaitege,Paul Maige na Paschal Frank.

Wengine ni Shafii Kilaba,Daniel Manyenye, Said Omary, Boniphace Swabi,Abdulsalam Katabazi,Alex Mwaisaka, Simon Cradius,Nelson Kitua,Alphonce Guleta,Tumaini Agustino,Aman Anuru na Wilson Koranti.

Nahodha wa Mbao FC, Henry Shindika alisema wataendelea kupambana kwa ushirikiano wao ili timu yao iweze kufanya vyema na kurejea ligi kuu.

 

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea ...

foto
Mwandishi: ALEXANDER SANGA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi