loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ng’arisha meno yako kwa stroberi

MENO meupe na safi ni moja ya vitu vinavyoongeza mvuto na urembo katika sura yako. Unapocheka au kutabasamu ukiwa na meno meupe na safi hupendezesha muonekano wa sura yako.

Kuna vitu vingi ambayo husababisha meno kupoteza mng’ao wake, lakini kuna njia nyingi pia za kurudisha mng’ao wa meno yako tena kwa kutumia vitu vya asili badala ya bidhaa za madukani zinazotengenezwa kwa kemikali.

Stroberi ni moja ya vitu unavyoweza kutumia kutakatisha meno yako na kurejesha mng’ao wake.

Ndani ya tunda hili kuna asidi ijulikanayo kitaalamu kama malic ambayo husaidia kuvunja chembe chembe zinazosababisha madoa, alama au uchafu kwenye meno wakati baking soda huchangia kung’arisha na kuyafanya meno kuwa meupe na kutabasamu kwa kujiamini na kupiga mswaki kutaondoa chembe za madoa ama uchafu kutoka mdomoni mwako.

Ponda stroberi na kutenga uji wa tunda lako na changanya na baking soda kutengeneza mchanganyiko mzito. Tumia mchanganyiko huo kwa kuweka kwenye mswaki laini na kusambaza kwenye meno.

Acha kwa dakika tano, kisha piga mswaki kwa dawa ya meno ili kuondoa mchanganyiko huo wa stroberi na baking soda. Kisha sukutua kwa maji safi

KATIKA kipindi cha miezi michache iliypopita, dunia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi