loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lissu apongeza Polisi kwa kazi nzuri

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), Tundu Lissu amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kujiendesha vizuri ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu yake vyema kwa wagombea wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Lissu alisema hayo jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza, huku akieleza kuendesha mikutano mingi ya kampeni kwa mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza.

Alikiri kuwa walipoanza mikutano ya kampeni, wao (Chadema) walikuwa na hofu ya kubughudhiwa na polisi akirejea kwenye kumbukumbu za chaguzi za nyuma zilivyokuwa.

“Polisi wametupa ushirikiano mkubwa sana, msafara wangu umekuwa ukisindikizwa na polisi kila mahali,” alisema na kuongeza kuwa hatua inayoonesha kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu, tofauti na chaguzi zilizotangulia, jeshi la polisi limetekeleza wajibu wake vizuri kwake, karibu kwenye mikutano yote ya kampeni zaidi ya 20 aliyofanya hadi sasa.

“Polisi wanafanya kazi nzuri sana wakati huu, wametekeleza wajibu wao vizuri sana kwa wagombea katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi,” alisema.

Lissu alisema kwenye mzunguko wake wa kwanza hadi wa tatu amefanya mikutano mingi ambayo imeungwa mkono na wanachama na wafuasi wengi, hali inayomthibitishia kuwa njia ya yeye kushinda iko wazi.

Alisema wingi wa watu unatokana na watu wenyewe kuhudhuria kwenye mikutano yake kwa utashi wao na mapenzi waliyo naye kwake.

Licha ya kulipongeza jeshi la polisi kwa kazi kubwa na nzuri, alikiri kutokea kasoro katika baadhi ya mikoa baada ya kuibuka vurugu za hapa na pale alipokuwa katika mkoa kama wa Kagera- Bukoba mjini.

Alisema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ataimarisha na kutengeneza uhusiano mwema na dunia sanjari na kuvutia wawekezaji wengi.

Lissu alisema hivi sasa Chadema ni chama bora cha siasa na kwamba imani yake kitashinda uchaguzi wa mwaka huu na kuchukua uongozi wa nchi, hasa mara baada ya kutengeneza programu ya “ Chadema ni msingi,” iliyowawezesha kusambaa kila mahali nchini.

WASIMAMIZI wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,wameonywa kujiepusha na ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi